HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 25, 2015

TAASISI YA UTAFITI YA VYUO VIKUU ESAURP YAANDAA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO MKOANI MBEYA

Mmoja wa wakufunzi wa masomo ya ujasiriamali Kutoka Chuo Kikuu Dar es salaam Profesa Humphrey Mushi akizungumza katika semina ya ujasiriamali inayotolewa na Taasisi ya utafiti ya vyuo vikuu vya afrika na kusini mwa Afrika ( ESAURP) kwa wafanyabiashara ndogondogo mkoa wa mbeya katika ukumbi wa shule ya St.Agrey jijini Mbeya Agosti 24 mwaka huu. (Picha Emanuel Madafa Mbeya).
Mwakilishi wa Taasisi ya Esaurp kutoka jijini Dar es salaam Ndugu Peter Celestine akizungumza katika mafunzo hayo ya siku tano yaliyolenga kuwapatia wajasiriamli hao Ujuzi ,Mbinu ,maarifa pamoja na stadi za biashara ili kuwezesha ukuaji wa biashara zao.
Baadhi ya wajasirimali kutoka maeneo tofauti tofauti Mkoani mbeya wakiendelea kupatiwa mafunzo.
Mmoja wa walimu katika mafunzo hayo Ndugu Upendo Mwinuka akizungumza na wajasirimali hao hawapo Pichani.
Afisa Mikopo kutoka Benki ya Posta Tanzania Mbeya( TPB) Ndugu Tresphory  Mtwele akizungumza na wajasirimali hao ili kuwashawishi kujiunga katika vikundi ili waweze kupatiwa mikopo ya riba nafuu na benki hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages