Mkuu wa
Mtandao wa Matawi ya Barclays Emmanuel Katuma (kushoto), Meneja Bidhaa wa Benki
hiyo, Valence Luteganya na Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa, Wateja Binafsi wa Benki ya
Barclays, Oscar Mwamfwagasi (kulia), wakionesha Kombe
la Ligi Kuu ya Uingereza (Barclays Premier League), litakalotembezwa katika
jijini Dar es Salaam na mashabiki wa soka kupata fursa ya kupigi nalo picha.
(Picha na Francis Dande)
Dar es Salaam, Tanzania
KOMBE la
Ligi Kuu ya Uingereza (Barclays Premier League), limetua rasm Jijini Dar es
Salaam jana, na kutembezwa maeneo mbalimbali kwa ajili ya mashabiki wa soka
kupiga nalo picha.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Barclays, Oscar
Mwamfwagasi alisema kuwa, kombe hilo lilianza kutembezwa jana katika maeneo ya
Uwanja wa Taifa, Mwembe Yanga na Mnazi Mmoja ambapo leo litaendelea kutembezwa.
Aliyataja
maeneo ambayo kombe hilo litatembezwa hii leo kuwa ni Uwanja wa Karume majira
ya saa 10:30 jioni huku Mlimani City kuanzia saa 5:00 asubuhi ambapo watakaa
saa moja na kuwataka wadau wa Soka hasa wale wapenzi wa timu za Uingereza
kujitokeza kwa wingi.
“Mbali
na Karume na Mlimani City hiyo kesho tunalipeleka Kinondoni Biafra, Slipway,
Manzese Darajani ili wapenzi wa soka waweze kupata fursa ya kupiga nalo picha,
wakiwa wamevalia jezi zao za timu wazipendazo kutoka Uingereza,”alisema.
Mwamfwagasi
alisema, katika zoezi hilo la kupiga picha, litakuwa bure kwani Barclays kwa
kutambua thamani ya wadau wao katika jamii ndiyo sababu ya kulileta kombe hilo,
licha ya kuwa huu ni mwaka wao wa mwisho kudhamini Ligi hiyo.
Aliongeza
kuwa, kwa heshima ambayo Tanzania imeipata ni kubwa sana kwani kombe hilo
Barani Afrika limetua katika nchi tatu pekee ambazo ni Uganda, Tanzania na sasa
linakwenda Afrika Kusini hii.
No comments:
Post a Comment