Na Mwandishi Wetu,
Hai
MKUU wa Mkoa
Kilimanjaro, Amos Makalla, amehudhuria halfa ya kuwapongeza walimu wilayani Hai,
mkoani humo, kwa kufanikisha ufaulu mzuri wa darasa la saba. Wilaya ya Hai
imepata nafasi ya kwanza kiwilaya mkoani Kilimanjaro, huku ikishika ikishika
nafasi ya nne kitaifa, jambo lililomkuna Mkuu huyo wa Mkoa Kilimanjaro.
Akizungumza katika halfa hiyo akiwa kama mgeni rasmi, RC Makalla, alisema kwamba Hai wanastahili pongezi na wanapaswa kuendelea kufanya bidii ili wazidi kufaulisha kiwilaya na kitaifa. Alisema kuna haja ya sekretarieti ya Mkoa huo na Halmashauri zote kujipanga na kushughulikia kero za walimu, madai ya mishahara, kupandishwa kwa madaraja pamoja na kujibu barua zao kwa wakati ili kuwapa moyo walimu wao hao.
“Mkoa wetu unawapa pongezi kubwa walimu wote wa wilaya ya Hai kwa kufanya kazi kubwa na nzuri ya kuhakikisha kwamba wanafunzi wenu wanafaulu vizuri. “Naomba muendelee kujituma katika ufundishaji wenu, huku nikiahidi ushirikiano mkubwa katika ofisi yangu na kwenu ninyi walimu ili kuleta ushirikiano mkubwa kati yetu,” alisema.
RC Makalla amekuwa akifanya ziara mbalimbali mkoani Kilimanjaro ili kuongeza ufanisi katika majukumu yao ya kila siku, huku wakiitumia vyema falsafa ya Hapa Kazi Tu, inayotumiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli.
No comments:
Post a Comment