HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 02, 2015

MASTAA KIBAO NDANI YA FILAMU YA HOME COMING

Mwongozaji mahiri wa filamu ya Homecoming inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni, Seko Shamte. Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Alkemist Media ina ujumbe wa kuhusiana na vishawishi vya rushwa pamoja na athari zake kwa wafanyakazi na jamii kwa ujumla.
Crew nzima pamoja na baadhi ya waigizaji
 Moja kati ya kamera kali zilizotumika
Kazi ikiendelea location

Na Mwandishi Wetu

WASANII mahiri wameshiriki kwenye filamu ya Homecoming inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni akiwamo Daniel Kijo, Mzee Chilo pamoja na mastaa wengine.


Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Alkemist Media ina ujumbe wa kuhusiana na vishawishi vya rushwa pamoja na athari zake kwa wafanyakazi na jamii kwa ujumla.


Kijo ambae anafahamika zaidi katika tasnia ya habari aliwahi kutangaza kwenye kipindi cha Daladala kinachorushwa na Star Tv, katika filamu hii ameigiza kama mhusika mkuu akitumia jina la Abel Mshindi.


Mzee Chilo ambae jina lake halisi ni Ahmed Olotu ameigiza kama mzazi wa Kijo ambae amekuwa akiishi kijijini miaka yote huku Mzee mwigizaji mwengine mahiri nchini Hashim Kambi ameigiza kama Mjomba wa Kijo.


Filamu inaanza kwa kumuonesha Kijo akitokea Marekani ambapo alisomea masuala ya fedha na kisha kurejea nchini na kuajiliwa katika kazi ya benki, kwa muda wote akiwa nchini amekuwa akiishi na mjomba wake ambae ni Kambi huku baba yake (mzee chilo) akiwa anaishi kijijini.


Kijo alijikuta akiingia katika janga la rushwa kutokana na kushawishiwa na shida za baba yake huyo aliekuwa akimtegemea kwa kila kitu huku pia kukiwa na mwanamke ambae nae alikuwa akitaka mahitaji.


Kutokana na changamoto za kimaisha Kijo alijiingiza katika janga la rushjwa na kujikuta akikamatwa na kufungwa.


Wengine katika filamu hiyo ni Susan Lewis maarufu kama Natasha, Uncle Mshindi, maarufu kama Hashim Kambi pamoja na Abby Plaatjes aliewahi kuwa mshiriki wa Big Brother Afrika.


Pia wapo akina Alpha Mbwana, Magdalena Munisi, Godliver Gordian, Michael Kauffmann na itaanza kuoneshwa kwenye kumbi ya cinema kabla ya kuingia rasmi sokoni. zaidi tembelea www.homecomingtz.com

No comments:

Post a Comment

Pages