Eliza Juma (30), mkazi wa Mtaa wa Mbwanga Manispaa ya
Dodoma anaomba msaada wa hali na mali kutoka kwa yeyote ataeguswa ili aweze
kufanyiwa upasuaji wa uvimbe tumboni ambao umekuwa ukiongezeka kila siku.
Akizunguma na waandishi wa habari mjini hapa Dodoma, alisema kuwa
uvimbe huo ambao umekuwa ukiongezeka kila siku umekuwa kikwazo kwake katika
kutekeleza majukumu yake ya kujipatia kipato.
Alisema kuwa uvumbe huo unaotokana na yeye kufanyiwa
upasuaji wa utumbo aliofanyiwa miaka miwili iliyopita kutokana na utumbo wake
kujikunja.
“Nilifanyiwa upasuaji wa utumbo miaka miwili
iliyopita katika hospitali ya mkoa wa Dodoma ambapo utumbo wangu ulikuwa
umejikunja lakini mara baada ya kufanyiwa upasujai huo kidonda kilianza kuwasha
na mimi nikawa napakuna ndipo pakaanza kuvimba hadi kufikia ukubwa huu unaouona
sasa” alisema Eliza.
Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo alikwenda
hopitali ya mkoa ili kuweza kuonana na daktali ambaye alimweleza kuwa tatizo
hilo linatokana na ngozi ya ndani kulika hivyo anatakiwa kufanyiwa upasuaji kwa
mara nyingine.
Aidha alisema kuwa kutokanana hali yake ya kiuchumi
na kiasi alicho ambiwa kulipia ili awze kufanyiwa upasuaji huo yeye hawezi kumudu
kwakuwa hana msaada wowote anaoutegemea zaidi ya wasamailia wema.
“Kiasi kinacho hitajika ili niweze kufanyiwa upasuaji
ni zaidi ya shilingi laki tatu na mie kama mnavyo hapa nilipo natunzwa na
wasamilia wema sina mama wala baba hivyo nawaomba wasamalia wema kunisadia ili
niweze kupata kiasi hicho kwaajili ya matibabu kabla tatizo halijawa kubwa
zaidi”alisema Eliza.
Alisema kuwa kwa yeyote atakaye guswa anaweza
kumchangia anaweza kuwasiliana naye kupitia namba ya simu ya mkononi 0678164633
ili aweze kupata kiasi hicho cha pesa na kupatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment