Kamshina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Suleiman Kova, akizungumza leo na waandishi wa habari, kuhusu kukamatwa kwa askari wa jeshi hilo na
wawili wa wanyamapori kwa tuhuma za kusababisha vifo vya watu wawili. (Picha na
Loveness Bernard)
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
JESHI la Polisi Kanda Maalum
ya Dar es Salaam, linawashikilia
askari Polisi wawili na askari wanne wa Idara ya wanyamapoli kwa tuhuma za
kusababisha vifo vya watu wawili waliotuhumiwa kujihusisha na ujangili.
Askari hao ni Boni
Mbange ambaye ni mkaguzi wa
Polisi, E.919D/SGT Filbert, askari wa wanyamapori ni Emmanuel Mbaga, Deogratias
Mwageni, Joseph Jimmy na Asubile Mwakyusa.
Watuhumiwa waliofariki
ni Yasini Rashidi (46) mkazi wa Mabibo na Samso Michael (46) mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, alisema awali waliwakamata
askari saba walioshiriki katika mauaji hayo lakini wakati wanahojiwa mmoja kati yao aitwaye F 5371 D/C Issa Kazimoto alitoroka mara baada ya tukio
hilo hivyo kumtaka alipo ajisalimishe.
Kova alisema taarifa za awali zinaonyesha askari hao pamoja
na wenzao wa idara ya wanyamapori kutoka
kikosi maalum cha kuzuia ujangili Tanzania
walikuwa wanafuatilia watu wa wili kwa tuhuma za ujangili.
“Msako ulipangwa kufanyika hapa jijini Dar es Salaam kuanzia
Desema 19 mwaka huu siku ya tukio baada ya asjkari hao kupata taarifa kutoka
kwa raia wema kwamba watu hao wanajihusisha na vitendo vya ujangili”.Alisema
Kamanda Kova.
Kova alisema Desemba
19 mwaka huu zilitolewa taarifa kituo
cha Polisi Magomeni kutoka kwa askari
waliokuwa Opareshini Sinza kwamba
watuhumiwa waliokuwa wanawafuatilia wamefariki katika harakati za ukamataji.
Kamanda Kova alisema uchunguzi wa awali katika tukio hilo
umebaini kuna utata tangu wakati wa ukamataji hadi vivyo vya marehemu hao
wawili na ndio sababu askari hao wa Polisi
na wa IDara ya wanyamapori wanashikiliwa ili kupata ukweli wa vifo hivyo
na uhalali wwa nguvu iliyotumika.
“Ukaguzi wa miili ya marehemu hao unaonyesha walipata
majeraha ya risasi hivyo wa kisayansi utafanyika ikiwa ni pamoja na kuwahusisha
madaktari bingwa wa uchunguzi wa miili (Forensis Doctors) vielelezo
vilivyotumika katika tukio hilo vikiwemo silaha na magari vinachunguzwa”alisema
Kamanda Kova.
Aliwataka wananchi wenye taarifa za ziada kuhusu tukio hilo
wajitokeze ili upelelezi ufanyike haraka na sheria ichukue mkondo wake.
No comments:
Post a Comment