HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 31, 2015

WAZIRI MBARAWA ATEMBELEA DARAJA LA KIGAMBONI

 Barabara zinazoingia katika Daraja la Kigamboni.
Mkurugezi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa alipofanya ziara ya kuangalia maendekleoa ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mattaka akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), wakati alipofanya ziara kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo linalotarajiwa kuanza kutumiaka rasmi ifikapo Februari 2016. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau.
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza wakati alipofanya ziara kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni ambalo linalotarajiwa kuanza kutumiaka rasmi ifikapo Februari 2016. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mattaka akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia)
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Hamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (katikati), wakati waziri huyo alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi  wa Daraja la Kigamboni  jijini Dar es Salaam. Kulia ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NSSF, Aboubakari Rajabu. 
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (katikati), akifafanua jambo wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau na kulia ni Ofisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uhusiano na Masoko wa NSSF, Salim Kimaro.
 Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mattaka (katikati) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau.
 Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau na Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mattaka wakitoa ufafanua kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto).
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mattaka akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa sehemu zilizosali ambazo zinazofanyiwa matengenezoya mwisho mwisho.
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akikagua ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam jana, daraja hilo linalotarajiwa kuanza kutumiaka rasmi ifikapo Februari mwakani. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NSSF, Aboubakari Rajabu, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau, Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mattaka na kushoto ni Mkurugenzi  wa Miradi na Uwekezaji NSSF, Yacoub Kidula.
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (katikati), akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NSSF, Aboubakari Rajabu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Hamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (kushoto) akiagana na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa mara baada ya kukagua ujenzi wa Daraja la Kigamboni linalojengwa kwa ubia kati ya NSSF na Serikali.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akiagana na Ofisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uhusiano na Masoko wa NSSF, Salim Kimaro.
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akiagana na Ofisa Uwekezaji Mwandamizi, Zaina Kambagha.
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akiagana na Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim mattaka.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja.
Waziri akiangalia maeneo yanayofanyiwa matengenezo.

DAR ES SALAAM, Tanzania

MENEJA Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karim Mattaka amesema kuwa ujenzi wa daraja hilo unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 31, 2016.

Mattaka aliyasema hayo jijini Dar es Salaam katika ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa alipotembele daraja hilo.
Alisema wanaamini kuwa watamaliza kazi hiyo kwa wakati na anawataka watanzania watarajie kuwa wataanza kulitumia daraja hilo ifikapo mwezi Februari mwaka huu.

“Tunatambua kuwa wananchi wanakiu ya kulitumia daraja hili na sisi tunawambia kuwa wasiwe na wasiwasi karibia tunamaliza yamebaki matengenezo madogomadogo ambayo tunaamini kuwa tutayamaliza kwa haraka,” alisema Mattaka.

Aidha alisema kutokwapo kwa wafanyakazi wenye ujuzi pamoja na kunyesha kwa mvua kubwa miezi iliyopita kumechangia wao kushindwa kumaliza kazi hiyo katika muda uliopangwa.

“Unajua hatuna wafanyakazi wa kutosha lakini pindi tunapohitaji sasa wale wenye ujuzi ili tuongeze nguvu wanakosekana jambo hili limechangia sana kuturudisha nyuma lakini pia kuna mvua kubwa ilinyesha kipindi cha nyuma imeharibu maeneo baadhi ambayo tulikuwa tumemaliza hivyo tumejikuta tunarudia upya kazi,” alisema.

Hata hivyo Mhandisi Mattaka alisema daraja hilo litakuwa na urefu wa mita 680 na njia zitakuwa sita yaani tatu kwaajili ya kwenda na nyingine tatu kwaajli ya kurudi.

“Licha ya daraja kuwa na mita hizi lakini barabara za awali ambazo zitakamilika zitakuwa ni kilomita 2 na nusu na zitakuwa na njia sita hizohizo, sisi tuhamu kubwa kuona watanzania walitumia daraja hili ndo maana tunafanyakazi usiku na mchana,” alisema.

Naye Waziri Mbarawa amemtaka Mhandisi huo kukamilisha kazi hiyo kwa muda uliopangwa ili wananchi waweze kulitumia na kuondoka na athari ya usafiri wanayoipata sasa.

Mbarawa ambaye alifika katika daraja hilo majira ya saa nne asubuhi na kutembelea mradi mzima amewataka wafanyakazi wote kwa ujumla kufanyakazi kwa bidii ili wakamilishe mradi huo kwa muda uliopangwa.

No comments:

Post a Comment

Pages