Mnamo tarehe 15 Julai 2015 Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa taarifa kwa umma kuhusu Watoa Huduma za
Maudhui ya Utangazaji (Redio na Televisheni) 40 waliokuwa wanadaiwa ada
mbalimbali zinazotokana na leseni zao. Aidha, tarehe 28 Septemba 2015 Mamlaka
iliwapa watoa huduma hao nafasi ya mwisho ya kulipa ada wanazodaiwa ifikapo 31
Desemba 2015. Hadi tarehe 4 Januari, 2016 ni watoa huduma 11 tu kati ya 40
wamelipa ada hizo kama walivyotakiwa kufanya.
Kuendelea kwa watoa huduma kutokulipa
ada za leseni ni ukiukwaji mkubwa wa masharti ya leseni chini yakifungu cha 21(g)
cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (The Electronic and Postal
Communications Act- EPOCA) Sura 306 ya Sheria za Tanzania. Kifungu 22(a) cha Sheria
ya EPOCA, pamoja na mambo mengine kinaipa nguvu Mamlaka kusimamisha au kufuta
leseni iwapo itathibitishwa kwamba mwenye leseni amekiuka kwa kiwango kikubwa
masharti ya leseni kama yalivyoainishwa kwenye kifungu 21 na inapothibitishwa
kwamba hakuchukua hatua kurekebisha ukiukwaji huo ndani ya siku 30 tangu apewe/apate
notisi/taarifa ya ukiukwaji huo.
Kufuatia kushindwa kwa watoa huduma walioorodheshwa hapa chini kulipa
ada zao za leseni, Mamlaka ya Mawasilianio Tanzania imesimamisha leseni zao na
kuzitaka redio na televisheni ambazo majina yao yanaonekana hapa chini kusitisha
mara moja utoaji wa huduma za utangazaji kwa miezi mitatu kuanzia tarehe 18 Januari
2016.
1.
BREEZE FM
2.
COUNTRY FM RADIO
3.
EBONY FM RADIO
4.
GENERATION FM
RADIO
5.
HOT FM RADIO
6.
IMPACT FM
7.
IRINGA MUNICIPAL
TV
8.
KIFIMBO FM RADIO
9.
KILI FM RADIO
10.
KISS FM RADIO
11.
KITULO FM RADIO
12.
MBEYA CITY
MUNICIPAL TV
13.
MUSA TELEVISION
NETWORK
14.
PRIDE FM RADIO
15.
RADIO 5
16.
RADIO FREE AFRICA
17.
RADIO HURUMA
18.
RADIO SENGEREMA
19.
RADIO UHURU
20.
ROCK FM RADIO
21.
SIBUKA FM RADIO
22.
STANDARD FM RADIO
23.
STAR TELEVISION
24.
SUMBAWANGA
MUNICIPAL TV
25.
TANGA CITY TV
26.
TOP RADIO FM
LIMITED
27.
ULANGA FM RADIO
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
inapenda kuwakumbusha wenye leseni wote kuhakikisha kwamba wanafuata Sheria na masharti
ya leseni zao ikiwa ni pamoja na kulipa ada za leseni kwa Mamlaka kwa wakati.
IMETOLEWA NA
Dr. Ally Y.
Simba
MKURUGENZI
MKUU
Januari, 2016
No comments:
Post a Comment