JESHI Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam limekamata
pikipiki zaidi ya 600 katika mikoa ya Kipolisi ya Ilala ,Temeke na Kinondoni
zikihusishwa na matukio mbalimbali ya uhalifu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kanda
hiyo, Simon Sirro alisema katika mkoa wa Temeke zimekamatwa pikipiki 130 ambapo pikipiki 55
zimelipishwa faini na pikipiki 75 zimeshikiliwa vituoni kwa uchunguzi.
Alisema kwa mkoa wa Kinondoni pikipiki zilizokamatwa ni 241
ambapo pikipiki 90 zimetozwa faini pikipiki 10 zimeachiwa huru baada ya
kujiridhisha na pikipiki 141
zinashikiliwa kwa uchunguzi.
Alisema kwa mkoa wa Ilala zimekamatwa jumla ya pikipiki 249
ambapo jumla ya pikipiki 134 zimelipa faini pikipiki 19 zimeachiwa huru na
pikipiki 95 zinashikiliwa kituoni kwa uchunguzi.
Sirro alisema kuhusu suala la uporaji kutumia pikipiki
unaotokea katika maeneo mbalimbali ya jiji hasa eneo la kibiashara la mlimani City
hatua za makusudi zimechukuliwa ikiwa ni
pamoja na kufanya Oparesheni maalum eneo hilo na kuona namna nzuri ya kuondoa
pikipiki maeneo hayo.
“Tumejipanga kuwasiliana na wamiliki wa taasisi za kifedha
kujiridhisha kama waajiriwa katika taasisihizo wanaweza kuwa wahusika kwa njia
moja au nyingine katika uhalifu huu unaohatarisha maisha ya wakazi wa Dar es
Salaam.”Alisema Sirro.
Katika hatua nyingine Kamanda Sirro alisema Desemba 12 mwaka
jana huko maaeneo ya Buguruni alikamatwa mtuhumiwa aitwaye Simba Said (44) ambaye ni mganga wa kienyeji mkazi wa vingunguti Koloni,
alipohojiwa alikiri kuwafanyia dawa majambazi kabla ya kwenda kufanya matukio
ya kijambazi.
Alisema mtuhumiwa huyo alisema walipanga kufanya tukio la
ujambazi maeneo ya Buguruni ,Polisi waliweka mtego na walipotaka kuwakamata
,walisitukia mchezo na kuwarushia risasi ndipo jambazi mmoja alijeruhiwa kwa
risasi na kupelekwa Amana ambapo baadae
alifariki dunia.
“Katika tukio hilo
majambazi wengine walifanikiwa kutoroka yakitumia pikipiki tatu,wakati
ufuatiliaji ukiendelea zilipatikana taarifa kuwa majambazi hayo yamekimbilia
maeneo ya Tabata na Polisi walifuatilia na kufanikiwa kukamata bunduki mbili
aina ya Pump Action ambazo namba zake zimefutwa na zikiwa zimekatwa mitutu.
Aidha Sirro alisema Januari 7 mwaka huu huko Gongolamboto
alikamatwa jambazi sugu aliyekuwa anatafutwa kwa muda mrefu aitwaye Mkama Hassan (32) mkazi wa mbagala maji matutu
na Gongolamboto ,alipopekuliwalea ili nyumbani kwake alikuwa na bastola aina ya
Chinese iliyofutwa namba ikiwa na magazine yenye risasi 7 mahhojiano
yanaendelea ili kuzalisha watuhumiwa wengine.
No comments:
Post a Comment