WAZIRI WA AFYA Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa
Ummy Mwalimu ametembelea jengo la zahanati ya Mpingi wilaya ya Songea
Vijijini na kuzungumza na wanakijiji wa eneo hilo.
Ziara hiyo ni moja kati ya kazi anazozifanya mkoani hapa kwa lengo la
kuzungumza na wananchi, watoa huduma na watumishi wa sekta ya afya ili
kuboresha huduma za matibabu na kuhamasisha wananchi kushiriki katika
shughuli mbalimbali za afya ikiwemo uchangiaji katika mifuko ya afya
Baada ya kufika kijijini hapo na kuona jitihada zilizofanywa na
Halmashauri na wananchi, Waziri Ummy aliwaahidi wananchi hao mabati na
misumari ili kuunga mkono ujenzi wa zahanati hiyo.
Mheshimwa Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wagenii kijijini Mpingi |
Baadhi ya wananchi wa Mpingi waliohudhuria kumlaki Waziri Ummy Mwalimu alipotembelea majengo ya zahanati yao. |
Waziri Ummy Mwalimu akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya, kutembelea majengo ya zahanati ya Kijiji cha Mpingi |
Mzee Mohamed Mussa, mkazi wa kijiji cha Mpingi akimshukuru Waziri Ummy Mwalimu kwa kutembelea kijiji chao na kutoa msaada wa bati na misumari ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji. |
No comments:
Post a Comment