HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 08, 2016

BENKI YA CRDB YATOA SHUKRANI KWA MUNGU

Mchugaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Msasani, Eliguard Meteli akiongoza ibada ya maalum ya Shukrani ya Mafanikio ya benki ya CRDB kwa kipindi cha mwaka 2015 iliyokwenda harambee ya kuchangia Shule ya Watoto na Miradi ya Maendeleo shuleni hapo iliyofanyika Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, (kulia) akipokea kadi ya mchango kutoka kwa Mchugaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Msasani, Eliguard Metili wakati wa harambee ya kuchangia Shule ya Watoto na Miradi ya Maendeleo shuleni hapo iliyofanyika Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, (kulia) akiwa katika ibada ya maalum ya harambee kuchangia ujenzi wa Shule ya Watoto na Miradi ya Maendeleo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Msasani, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulikia Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhayay. 
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa  (katikati) akiwa katika ibada hiyo.
 Ibada ikiendelea.
 Mchungaji Eliguard Metili akitoa baraka.
 Kwaya ya Ukombozi Choir ikiimba nyimbo za kumsifu mungu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akitoa Sadaka wakati wa ibada ya Shukrani ya Mafanikio ya benki ya CRDB kwa kipindi cha mwaka 2015.
Baadhi ya waumini wakiwa katika ibada hiyo. wa pili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu.
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa  akigawa chakula kwa mtoto aliyehudhuria ibada hiyo.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela akitoka kanisani mara baada ya kumalizika kwa ibada.

No comments:

Post a Comment

Pages