Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama.
Na Mwandishi Wetu
WADAU
wa muziki wa injili wa jijini Dar es Salaam wameingiwa na hofu juu ya Tamasha
la Pasaka kama mwaka huu litafanyika ama
litaishia mikoani kwa mara
ya
kwanza katika historia yake tangu lianzishwe mwaka 2000.
Hofu
ya wadau hao Tamasha hilo inatokana na hatua ya waratibu
wake Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam kuitaja maeneo ya
mikoa ya Mwanza na Geita pekee, hivyo
wapenzi na mashabiki wa jijini Dar es
Salaam kuhoji kulikoni.
Mkazi wa Temeke jijini
Dar es Salaam, Anastazia Ferdinand Malinza wa Machimbo, alisema ameshtushwa kuona waratibu wanataja tamasha hilo mikoani
tu na kujiuliza kuna kitu gani kimetokea.
“Kwa
miaka mingi tumezoea liwe Tamasha la Pasaka au Krismasi, limekuwa likianzia
jijini Dar es Salaam ndipo liende kwingineko mikoani kulingana na uwezo wa
waratibu, lakini safari hii tunasikia tu Mwanza, Geita na kwingine katika Kanda
ya Ziwa,” alisema Annastazia.
Alisema
akiwa mpenzi na shabiki wa tamasha hilo ambalo limekuwa likifanyika Ukumbi wa
Diamond Jubilee kwa miaka mingi na baadaye kuhamia uwanja wa Taifa kwa miaka ya
hivi karibuni, kama litafanyika mikoani tu, wao wa Dar es Salaam watakuwa
hawajatendewa haki.
“Kama
Msama na Kamati yake wataamua tamasha hilo
lifanyike mikoani tu, jamani watakuwa hawajatutendea haki kabisa kwa sababu ni
tukio ambalo tumelizoea kila mwaka tumekuwa tukienda kupata baraka na watoto
wetu,” alisema.
Alisema
kama kweli Tamasha hilo halitafanyika jijini Dar es Salaam , litakuwa ni pigo kwa wapendwa ambao mara
zote wamekuwa wakiliunga mkono tukio hilo
ambalo mbali ya kubeba ujumbe wa neno la Mungu, pia kuyafariji makundi maalum.
Alipotafutwa
kwa njia ya simu jana kuhusu maoni hayo, Msama alisema ni kweli Tamasha hilo limekuwa likianzia jiji Dar es Salaam kila mwaka kabla ya kwenda
mikoani, lakini mwaka huu walifanyika mikoani tu kutokana na sababu maalumu.
Alisema,
sababu ya kuifanya hivyo ni kutokana na matamasha mengi kufanyika
jijini
Dar es Salaam ,
hivyo mpango uliopo ni kuhamia mikoani kwa miaka mitatu mfululizo na kuwataka
wadau wa mikoani kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono.
No comments:
Post a Comment