HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 22, 2016

MKUU WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA ASIMAMISHWA KAZI KWA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA UMMA

Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Said Nassoro (kushoto), akielekea Ofisi kwake, baada Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki kutangaza kumsimamisha kazi katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Loveness Bernard)
Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki akitangaza kumsimamisha kazi Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Said Nassor pamoja na Kaimu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha, Joseph Mbwilo na Mtendaji wa Chuo cha Tabora Silvanus Ngata wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
 
Na Mwandishi Wetu

WAZIRI  wa nchi,ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi  wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki amemsimisha kazi Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Said Nassoro kutoka na uzembe ulioisababishia serikali  hasara  ya  bilioni 1.
 
Sambamba na Mkuu huyo wa Chuo Waziri Kairuki amewasimamisha  kazi Kaimu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha, Joseph Mbwilo na Mtendaji wa Chuo hicho tawi la Tabora, Silvanus Ngata.
  
'amesema amefikia hatua hiyo ya kuwasimamisha kazi watumishi hao baada ya kubaini utendaji usioridhisha katika vyuo hivyo'.
 
Amesema Nassoro amemsimisha kazi baada ya kushindwa kuwasimamia watumishi wa chini yake katika  chuo hicho.
 
'Mwaka  2011 hadi  2013, Silvanus Ngata aliongeza gharama za ujenzi wa jengo la chuo hicho tawi la  Mtwara tofauti na fedha iliyokuwa imepangwa'.  

'Chakushangaza, huyu Nassoro ambaye ni mkuu wao,  baada ya kugundua kosa hilo alishindwa kumuwajibisha na badala yake aliamua kumhamishia tawi la chuo cha Tabora. Sasa mimi nawasimamisha kazi wote.'Amesema Kairuki
 
Pia Waziri Kairuki amesema amemsimamisha Mbwiro kutokana na matumizi mabaya ya fedha za chuo ambapo mwaka 2013 alitumia vibaya fedha za ada za wanafunzi  kiasi cha shs. bilioni 1, lakini licha ya ubadhilifu huo, Nassoro alimteua Mbwiro kuwa Kaimu Mkuu wa Chuo kwa upande wa fedha.' alisema Waziri Kairuki.

No comments:

Post a Comment

Pages