NA KENNETH NGELESI,TUNDUMA
WAZAZI wenye watoto wanao soma shule ya Msingi Katete kata ya Mpemba katika wilaya ya Momba mkoani
Songwe wameamua kuchangishana pesa shilingi 2,000 kwa kaya ili kukamilisha
ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa kutokana na ongezeko la wanafunzi katika shule
hiyo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Daniel
Dilunga alisema Wananchi walifikia hatua ya kuchanga kiasi hicho cha fedha
kutokana na shule hiyo kuwa ongezeko kubwa na wanafunzi wa darasa la kwanza
mwaka ambapo kutokana na sera ya elimu kutolewa bure shule hiyo imeandikisha
wanafunzi 619 wa darasa la kwanza mwaka huu kutoka wanafunzi 230 mwaka jana.
Diluna alisema kuwa shule Katete ina wanafunzi 2169 wanaotumia vyumba 11
vya madarasa ikiwa na upungufu vyumba vya madarasa 25 hivyo kusababisha
msongamano wa wanafunzi hali iliyo sababisha kufanya machango huo ili watoto
maali pa kusomea.
‘Bado tuna changamoto kubwa hasa katika suala la
miuondombinu hasa kulingani na watoto niliyo nao hapa,mahitaji ya madawati ni
621 yaliyopo ni 251,mahaitaji ya madarasa 36 yaliyopo ni 11 matundu ya vyoo
mahitaji ni 99 lakini kwa sasa ninamatundu 15 tu hivyo hali ni mbaya niombe
wadau watakao gunswa na hilo kma ambayo ameguswa mbunge wetu ili vijana wetu
wapate elimu katika mazimngira mazuri’ alisema Dilunga
Mbali na hilo Dilunga alitoa ufafanuzi huo wakati akipokea
mifuko hamsini (50) ya Saruji ilitolewa na Mbunge wa jimbo la Tanduma Frank
Mwakajoka kwa ajili ya ujenzi ambapo Mwalimu huyo alisema kuwa Changamoto
nyingine inayo ikabili shule hiyo ni uhaba wa vyoo, madawati na nyumba za
walimu ambazo zimekuwa zikiikabili shule hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1975
‘Msongamano huo umetokana na ongezeko la wanafunzi baada ya
tamko la serikali chini ya Rais Dkt John
Pombe Mgafuli la elimu bure kuanzia msingi hadi kidato cha nne,lakini pia hamasa
mbalimbali zinatolewa na viongozi wa Serikali
pamoja na wanasiasa vikwemo ni pamoja na vitisho vya kuwachukulia hatua za
kinidhamu wazazi watakao shindwa kuwa peleka watoto wao shule’ alisema Dilunga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa Mpembe Gasper Mwakalinga
ilipo shule hiyo ambaye anabainisha kuwa wazazi wenyewe wamelidhia kutoa
michango pasi kushurutishwa huku akishukuru msaada uliotolewa na Mbunge wa
jimbo la Tunduma Frank Mwakajoka ambaye kawa unga mkono kwa kuwapa mifuko 50 ya
saruji kwani itapunguza makali ya kufanikisha zoezi la ujenzi wa madarasa hayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji huyo Ally
Mwafongo ambaye alikabidhi mifuko hiyo kwa niaba ya Mbunge alipongeza juhudi zilizo
fanywa na wazazi wanafunzi wanaso soma shule hiyo ambao wameamua
kuunganisha nguvu kazi ili kuhakikisha watoto wao wanasoma katika mazingira
mazuri.
No comments:
Post a Comment