Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa
habari juu ya ufunguzi wa duka la simu za mkononi na huduma za
matengenezo ya simu Samora jijini Dar es Salaam. Wananchi wametakiwa
kutumia simu orijio ili kuepuka usumbufu utakojitokeza kwa kuzimwa kwa
simu feki ifikapo June mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzindizi wa duka jipya la kampuni ya
huwawei mkuu wa mkoa bwana said Meck sadiki amesema kuwa zoezi la
uzimaji wa simu hizo uzimaji huo haujaanzia hapa nchini bali limefanyika
katika nchi nyingi zilizoendelea.
Aidha Meck Sadick amesema kuwa ni wakati sasa wa makampuni ya simu
kuakikisha yanatengeneza simu imara na kuwa na mafundi wa uhakika ili
kupunguza usumbufu unaojitokeza kwa wateja wao.
Meneja
Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang, akizungumza na wandishi wa
habari hawapo picha juu ya mbinu zilizotumika na kampuni ya Huawei,
ambapo wanajitahidi kuwa Karibu zaidi na wateja wake na kuendeleza
zaidi uzoefu katika matumizi ya bidhaa za Huawei.
"Ili
kuwahudumia Zaidi wateja wake Huawei tume fungua Maduka Mapya ya Huawei
pamoja na huduma za matengenezo ya simu za mkononi jijin Dar es
Salaam,baada ya kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa za Huawei na
kuhakikisha kuwa na vifaa vya uhakika na orijino vinapatikana kwa wateja
wao kirahisi.jijini Dar es Salaam" amesema Zhangjunliang.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akipatiwa maelekezo na Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu ,
Samora jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment