NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye (pichani) amepewa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la
Pasaka litakalofanyika siku ya Machi 27 katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini
Mwanza.
Mwenyekiti wa Kamati ya maaandalizi ya
tamasha hilo, Alex Msama alisema kwamba Waziri Nape amepewa heshima hiyo
sio tu kutokana na uhusiano uliopo kati ya wizara yake na tukio hilo, pia udau wake
na masuala ya nyimbo za injili kwa asili.
Msama alisema tukio hilo litakaloanzia mkoani
Geita hapo Machi 26, baada ya Uwanja wa Kirumba, jijini Mwanza, uhondo huo wa
nyimbo za injili utahitimishwa hapo Machi
28 katika mji wa Kahama.
Ametoa shukrani kwa Waziri Nape kukubali
kubeba jukumu hilo akiamini pia wadau wa muziki wa injili watajitokeza katika
tamasha hilo katika maeneo hayo matatu litakapofanyika kwa siku tofauti ambapo
safari hii ni rasmi kwa Kanda ya Ziwa.
Alisema kamati yake inaendelea maandalizi
ya kuelekea tamasha hilo ambalo litashirikisha waimbaji mbalimbali hapa nchini.
“Maandalizi kuelekea Tamasha la Pasaka
yanaendelea vema, hivyo wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wajiandae kupokea
ujumbe wa neno la Mungu kupitia viongozi wa dini na waimbaji wa muziki wa
Injili,” alisema Msama.
Msama alisema baadhi ya waimbaji waliothibitisha kushiriki tamasha hilo wameanza
kujiweka sawa ambao ni malkia wa muziki
wa injili, Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone na Jesca BM Honore.
Wengine ni Christopher Mwahangila, Joshua Mlelwa, Sifael
Mwabuka, Jenipher Mgendi, Kwaya ya AIC Makongoro ya Arusha na Kwaya ya
Wakorintho Wapili ya Njombe.
Tamasha hilo ambalo limebena malengo
kibao likiwemo la kupata fedha kwa ajili ya kusaidia makundi maalumu kama
Yatiba, walemavu na wajane, kiingilio ni sh. 5,000 kwa wakubwa na kwa watoto
shilingi 2000.
No comments:
Post a Comment