HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 16, 2016

WAFANYAKAZI AICC WALA KIAPO CHA AHADI YA UADILIFU

Wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) wakila kiapo cha Uadilifu kabla ya kujaza fomu za ahadi ya uadilifu kwa watumishiwa Umma.
MkurugenziMwendeshajiwaKituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), ndugu Elishilia Kaaya akiweka saini fomu za ahadi ya uadilifu za baadhi ya wafanyakazi wa AICC baada ya wafanyakazi hao kuapa na kuzijaza.
Afisa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi Umma ndugu Hendry Sawe akitoa mada juu ya Maadili kwa Viongozi wa Umma na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishiwa Umma muda mfupi kabla ya wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kujaza fomu za ahadi ya uadilifu. 

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), ndugu Elishilia Kaaya akiongea na wafanyakazi kabla ya kuapa na kujaza fomu za ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa Umma. Katikati ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa AICC, ndugu Savo Mungóngó na kulia ni Afisa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi Umma, ndugu Hendry Sawe.


Arusha, Tanzania

Wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) leo wameshiriki katika zoezi la ujazaji wa fomu za ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma.

Zoezi hilo limeongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC ndugu Elishilia Kaaya pamoja na Maofisa kutoka Sekretarieti ya Maadili yaViongozi wa Umma Kanda ya Kaziskazini.

Akizungumza katika zoezi la ujazaji wa fomu hizo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC amesema kwamba zoezi hilo ni utekelezaji wa agizo la serikali ambalo wafanyakazi wote wa umma na taasisi zake kuhakikisha wanajaza fomu za uadilifu kama ilivyoelekezwa katika Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma na mbambili (2) wa mwaka 2015.

“AICC ni taasisi ya umma hivyo wafanyakazi wote wa Kituo hiki wana wajibika moja kwa moja kujaza fomu hizi za uadilifu kwa mujibu wa agizo la serikali”, alisemaKaaya.

Kwaupande wake, Afisa Maadili kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaziskazini, Henry Sawe, ameipongeza AICC kwa kuitikia wito wa kujaza fomu za uadilifu kwa kila mfanyakazi na kwamba ofisi yake inaendelea na zoezi hilo kwa taasisi zingine za umma na binafsi ambazo bado hazijatekeleza zoezi hilo.

“Tumefarijika kuona kuwa AICC imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza agizo la serikali kwani kila mtumishi wa umma anapaswa kujaza fomu hii ili kuhamasisha watumishi kuwa waadilifu, wawazi, wawajibikaji na wenye kuzingatia weledi katika kuhudumia umma”, alisistizaSawe.

AICC ni taasisi ya serikali iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ambapo taasisi hiyo inajishughulisha na kutoa huduma za mikutano, upangishaji wa ofisi na nyumba pamoja na kutoa huduma za afya kupitia hospitali yake ya AICC iliyopo jijini Arusha.

Kituo hiki pia kinasimamia Kituo kingine cha Kisasa cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) kilichopo Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages