Na Mwadishi Wetu
CHAMA cha Wananchi CUF kinatarajiwa kukutana katika kikao cha Baraza Kuu Taifa la Uongozi jumamosi ijayo, ajenda Kuu ikiwa ni hali ya kisiasa Zanzibar baada ya uchaguzi wa marudio uliyofanyika Machi 20, mwaka huu.
Kikao hicho ambacho kinakuja huku baadhi ya wanachama wa chama hicho wakionekana kama wamechanganyikiwa kutoka na kususia Uchaguzi huku na kupelekea CCM kujinyakulia ushindi katika nafasi zote kinategewa kutoka na azimio zito juu ya hali ya kisaisa visiwani hapa.
“Ndio tunategemeo kukaa siku ya Jumamosi mwishoni wiki hii na suala la hali ya kisaisa litachukua mda kubwa kuzungumzwa” kilisema chanzo chetu cha kuaminika.
Chanzo hicho kilisema pia wajumbe watajadili mambo mengine, wakati huu ambapo wananchi wanahamu ya kujua kinachoendelea katika chama kwa hiyo kupitia baraza hilo wanategemea kuwapa mwanga wapi wanaelekea.
Kilifahamisha kwamba kutokana na hali ilivyo sasa hasa tangu kutangazwa Dk. Ali Muhammed Shein kuongoza tena Zanzibar wanachama wanachama wao hawajui nini hatma ya chama chao pamoja wao wenyewe.
“Lazima tutoke na kitu ambacho kitaweza kuwanyanyua kivyengine kabisaa wafuasi wetu kwani hatuwezi kustahamilia na dhulma hii hivi hivi” kilitueleza chanzo chetu.
Hali ya wasi wasi na ghofu kubwa imetanda miongoni mwa wanacuf kutokana kuongezeka kukamatwa kwa viongozi pamoja na wanachama wa CUF katika maeneo mbali mbali Visiwani hapa.
Kiujumla hali ya kisiasa viswani hapa imekuwa ya kuti hofu baadhi ya viongozi na wanachama maarufu wa CUF na kupelekea wengine kuaza kukimbia majumba yao.
Tokea kabla na baada ya uchaguzi wa marejeo takwimu zinaonesha wanachama zaidi ya 80 wamekamatwa kwa tuhuma mbali mbali ikiwemo, Uchomaji moto majengo ya serikali na makaazi ya watu pamoja na uripuaji na utegaji mabomu katika maeneo tafauti Unguja na Pemba.
Kutokana na kamata kamata hiyo baadhi wana CUF wanataka kujua hatma yao nini na nini chama chao kinawaeleza.
Katika mitaa mingi hasaa maeneo ambayo chama hicho kilijinyakulia majimbo katika uchaguzi ambao ulifutwa hapo October 25 mwaka jana wamekuwa wakijiuliza wapi wanaelekea.
Kikao cha mwisho cha baraza Kuu kilicho fanyika kilikaliwa Novemba mwaka jana ambacho kiliamua kususia kwa uchaguzi wa marejeo ambayo ulifanyika Mach 20 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment