UONGOZI wa
Benki ya Barclays Tanzania umewahakikishia wateja wake kuwa benki hiyo haiwezi
kufungwa kwa kuwa ina uwezo wa kuendelea kutoa huduma bora za kifedha.
Hivi
karibuni zilienea taarifa ya Benki hiyo kusitisha huduma zake kwa nchi za
Afrika ikiwemo Tanzania baada ya kudaiwa kupata hasara ya zaidi ya Euro Milioni
500.
Akizungumza
na wanahabari Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Tawi la Tanzania, Kihara Maina
alikiri kuwepo kwa taarifa ya benki hiyo kusitisha kutoa huduma lakini hivi
sasa wana uwezo wa kifedha wa kuendelea kutoa huduma zao.
Alisema
katika taarifa hiyo inaeleza kuwa pato lao limekuwa kwa asilimia 10 katika soko
la hisa la Afrika Kusini hivyo waliwataka Watanzania kuondoa hofu kwa kuwa
fedha zao zipo salama.
“Benki yetu
inayofuraha kuwatangazia kuwa pato letu limeongezeka kwa asilimia 10 kwa mwaka
uliomalizika Desemba 31 mwaka 2015, hiyo inatokana na utendaji imara,” alisema.
Alisema kuwa
benki hiyo itaongeza mkazo katika kusaidia na kushughulikia baadhi ya kero
zinazolikabili bara la Afrika ikiwemo ukosefu wa ajira, umaskini, kuhakikisha
upatikanaji wa elimu na huduma bora za kifedha.
“Hatuna
shaka kwamba miaka mitatu ya mkakati wetu ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2014
umetuweka katika nafasi nzuri zaidi kuliko mwanzo hivyo tuna jukumu kubwa la
kutoa huduma bora kwa jamii,” alisema.
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maim akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam, kuhusu ripoti ya Fedha ya mwaka 2015 ya benki
hiyo Afrika. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Masoko wa benki hiyo, Joe Bendera. Kwa
mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Barclays Afrika, Maria Ramos amesema kuwa benki hiyo
imeongeza faida yake hadi kufikia asilimia 8 sawa na R29.5 bilioni, pamoja na
kukanusha taarifa za kusitisha kutoa huduma za kifedha Barani Afrika. Kushoto
ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Joe Bendera. (Picha na
Francis Dande)
No comments:
Post a Comment