John Wang, Meneja Masoko wa kampuni ya Sunshine Gypsum Limited ya Kibaha mkoani Pwani, akionyesha vipande vya gypsum vinavyotengenezwa na kampuni yake. John Wang alikuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa umeme katika manendeleo ya sekta ya viwanda hapa Tanzania.
Na Mwandishi Wetu
Kuimarika sekta ya Umeme ni ukombozi pekee wa maendeleo ya viwanda katika kujenga uchumi imara na endelevu nchini Tanzania.
Mwekezaji wa kiwanda cha Sunshine Gypsum Limited cha Kibaha mkoani Pwani, John Wang ametoa ushauri huo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
John Wang ambaye ni Meneja Masoko wa kiwanda hicho amesisitiza kuwepo kwa mikakati ya makusudi wa kuondoa tatizo la umeme linalokabili sekta ya viwanda nchini Tanzania.
Amesema kuwa kwa sasa sekta ya viwanda inaongezeka kwa kasi sana na kufanya uzalishaji kuwa mkubwa katika miaka kumi inayokuja.
Licha ya kukiri kuwepo kwa mikakati ya kitaifa ya kuimairisha sekta ya umeme, John Wang amesema kuwa kasi ya mendeleo ya viwanda hapa Tanzania inaongezeka kwa kasi kubwa kuliko mikakati hiyo.
Meneja Masoko huyo amedai kuwa serikali lazima itoa msukomo wa kutosha katika kuimarisha sekta hiyo ya viwanda inayozalisha bidhaa bora hapa Tanzania.
Amesema kuwa viwanda hapa Tanzania havina budi kupata msaada wa upendeleo hususani katika sekta nyeti hiyo ya umeme.
“ Kwa kweli umeme ni tatizo linalotakiwa kuangaliwa kwa macho ya serikali kwa sababu ni msiba kwa wenye viwanda hapa nchini”, amesema John Wang
John Wang pia maelalamikia tatizo la usafirishaji wa mali ghafi kutoka sehemu inakopatikana kwenda eneo la kiwanda.
Amesema kuwa usafirishaji wa mali ghafi ni eneo lingine linalotakiwa kuangaliwa kwa macho mawili na serikali kwa sababu bidhaa zinacheleweshwa kufika eneo la viwanda kwa sababu ya mfumo mbovu wa usafirishaji hapa nchini.
Kuhusu wafanyakazi wa kitanzania waliopo katika kiwanda cha Kibaha mkoani Pwani, John Wang amesema kuwa anatarajia kuwapa mafunzo zaidi kwa wafanyakazi wake 100 wa kiwanda hicho.
Amesema kuwa anatarajia kuleta mitambo ya kisasa katika kiwanda chake na kufanya uzalishaji uongezeke mara dufu katika mwaka 2016 hadi 2018.
No comments:
Post a Comment