Na Mwandishi Wetu
UKOSEFU wa ‘dustibin’ za kuhifadhi takataka katika
mitaa mbalimbali ikiwemo Kivukoni jijini Dar es Salaam kumekuwa chanzo cha
mlundikano wa takataka katika mitaa hiyo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivukoni Gasper
Makame, aliyasema hayo wakati akisimamia kazi ya usafi katika mtaa huo,
inayofanyika kila wiki ya mwisho wa mwezi.
Utaratibu huo ni utekelezaji wa agizo la Rais John
Magufuli, la kubadisha Siku ya Desemba 9
kuwa ya Usafi baadala ya kuwa Siku ya maadhimisho ya Uhuru.
Makame, alifikia hatua hiyo baada ya wakazi wa mtaa
huo waliyokusanyika kwa ajili ya kufanya usafi kulalamika kuwa wanakabiliwa na tatizo
la dustibin za kuhifadhia takataka zinazozalishwa kila siku.
“Hicho wanachosema wananchi ni sahihi kinachotakiwa
hapa ni tuhamasishe wale wenye uwezo na wale ambalo hawana uwezo
tusaidiane angalau tuweke sh 200 kwa
kila mmoja ili tupate dustibin, dustibi ni shidana tatizo kweli,”alisema
Makame.
Hata hivyo, Makame alisema pamoja nakazi hiyo ya
usafi kwenda vizuri lakini bado wanakabiliwa na tatizo la kufanyia katika
kipande cha mita 60 ambacho kiko chini ya Bandari.
Alisema kipande hicho kiko ufukweni mwa bahari
ambapo kimezunguushiwa uzio ambao unawafanya washindwe kuingia bila ya idhini
ya uongozi wa Bandari.
“Tulifika pale tukashindwa kuingia lakini kwa vile
kile kipande nichao basi ni vema wakaoesha mfano kwa kukiweka katika hali ya
usafi, lakini kuna baadhi ya vijana wanaokaa pale (Mateja), wenyewe wanaiomba
bandari iwaletee vifaa wapkifanyie usafi,”alisema Makame.
Aidha, alisema wauza matunda kwa mikokoteni
wamekuwa kero kubwa katika mtaa huo, kwani wamekuwa chanzo cha uzalishaji wa
takataka ambazo baada ya shughuli zao huzitekelekeza na kuzifanya zinaoza na
kusabisha harufu mbaya katika maeneo husika.
Makame, alisema katika kukabiliana na tatizo hilo,
hadi sasa wamefanikiwa kukamata baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la Motel
Agip na kuzuia mikokoteni yao katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa kwa ajili ya
kuwachukulia hatua za kisheria.
Kuhusu kupigwa marufuku matumizi ya pombe
inayojulikana kwa jina la Viroba, kutokana na vipakti vyake kuzalisha uchafu,
Makame alisema inategeme kauli ya uongozi wa juu kwa vile watakaposema wao serikali
ya mtaa kwa kushirikiana na wananchi hilo litafanikiwa
Awali wakazi wa mtaa huo waliomba serikali isambaze
dusbin nyingi katika mitaa ambazo zitawafanya wananchi kutupa takataka zao humo
huku piawakiomba kupigwa marufuku pombe ya kiroba ambayowamedai vifungashio
vyake vimekuwa vikichafua mazingira kwa kiasi kikubwa.
No comments:
Post a Comment