Mkurugenzi wa
Huduma kwa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Valerian Mablangeti
akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari muliofanyika leo jijini Dar es Salaam nane, kuhusu mkutano wa 8 wa wadau wa mfuko huo utakaofanyika jijini Arusha
kuanzia Machi 10-11. Kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James
Mlowe. (Picha na Francis Dande).
Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe akifafanua
jambo jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mkutano wa nane wa wadau mfuko huo
utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Machi 10-11. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Huduma kwa Wanachama wa LAPF, Valerian Mablangeti.
Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe akifafanua
jambo jijini Dar es Salaam, kuhusu mkutano wa nane wa wadau mfuko huo
utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Machi 10-11. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Huduma kwa Wanachama wa LAPF, Valerian Mablangeti.
NA MWANDISHI WETU
JUMLA ya wanachama 246 wamefaidika na mkopo wa upimaji ardhi ambao
umekuwa ukitolewa na Mfuko wa Hifadhi wa LAPF kwa wanachama wake.
Akizungumza jana, Meneja Masoko na Mahusiano wa mfuko huo, James Mlowe,
alisema utaratibu huo ulianza Novemba, mwaka jana na tayari Sh. Milioni 160
zimekwisha kutumika.
Alisema lengo la kubuni mradi huo ambao wanashirikiana na Benki ya NMB,
ni kuwaepusha wanachama wao kutoishi katika makazi holela.
Aidha, alisema mafanikio mengine ambayo mfuko huo umeyapata ni pamoja na
kukua kwa thamani kutoka Sh. Trilioni moja mwaka jana hadi Sh. Trilioni 1.87
mwaka huu, huku wakiwa na wanachama 160,000.
Akizungumzia mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika Machi 10 hadi 11 jijini
Arusha, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama, Venerian Mablangeti, alisema huo ni
mkutano wa nane tangu waanze.
Mablangeti alisema kufanyika kwa mikutano hiyo licha ya kutimiza sheria
ya uundwaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii, umelenga kuwakutanisha wanachama na
kuweza kujua taarifa mbalimbali kuhusu michango yao.
No comments:
Post a Comment