HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 12, 2016

Benki M yazidi kupasua anga

Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso akifafaanua jambo wakati akitangaza ripoti ya fedha ya robo ya kwanza ya mwaka 2016 jijini Dar es Salaam, ambapo imeweza kupata faidi ya shs. Bilioni 7.4. (Picha na Francis Dande)

 Mkurugenzi Mkuu Bank M, Jacqueline Woiso akifafaanua jambo wakati akitangaza ripoti ya fedha ya robo ya kwanza mwaka 2016 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Mteule wa Benki M, Jacqueline Woiso.
 NA MWANDISHI WETU

BENKI M Tanzania PLC, imefunga robo mwaka robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2016 kwa mafanikio baada ya kupata ongezeko kubwa katika waraka wake wa mizania, pia kwa upande wa faida.

Akizungumzia mwendo wa Benki hiyo, Mkurugenzi Mkuu Mteule wa Bank M, Jacqueline Woiso, amesema leo, ni faraja kubwa kwao kwa sababu imezidi kupata mafanikio.

Alisema, Benki hiyo yenye umri wa miaka tisa sasa, imeweza kupata faida kabla ya kodi ya shilingi za kitanzania Bilioni 7.4 kwa kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka kutoka shilingi bilioni 6.13 katika kipindi cha kama hicho kwa mwaka uliopita.

Aliongeza, fedha kwa kipindi cha miezi mitatu inayoishia Machi 31, 2016, sehemu kubwa ya faida ya hiyo imetokana na riba ya mikopo ambayo kwa ujumla wake imefikia kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 22.11.

Kwamba, kiasi hicho, ni sawa na ongezeko la asilimia 32 ikilinganishwa na faida iliyopatana mwaka jana katika kipindi kama hicho. 

Aidha, faida itokanayo na huduma za kibenki imeripotiwa kufikia kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 6.6, ikiwa ni asilimia 15 zaidi ikilinganishwa na faida ya kipindi kama hicho kwa mwaka jana.

Kwa upande mwingine, taarifa hiyo imesema hadi kufikia Machi 31, 2016, rasilimali za benki zimeongezeka kufikia kiasi cha shilingi bilioni 889.11 ikiwa ni ongezeko la asilimia 22 kutoka Desemba, 2015.

Pia, kwa katika kipindi kama hicho, amana zimeongezeka kufikia shilingi Bilioni 746.49 sawa na asilimia 19.

Alisema, mipango inaendelea kuongeza mtaji tete wa benki kupitia wekezo binafsi na hisa tangulizi, vyombo hivi vitasaidia katika ongezeko la mtaji kwa kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 50.

Aliongeza kuwa, mpango wa kuongeza mtaji umepangwa kutelezwa katika robo ya pili na ya tatu ya mwaka huu wa fedha kutegemea na idhini ya vyombo vya usimamizi. 

Kwa upande wa bidhaa, alisema Bank M ipo katika mchakato wa kuongeza bidhaa mbili mpya katika soko ambazo ni Money Moja kwa Moja itakayowezesha wateja kupakia hundi kwa ajili ya malipo moja kwa moja kutoka katika ofisi zao bila kutembelea matawi ya benki kuweka hundi.

Alisema, bidhaa nyingine ni Cash Management System itakayowasaidia wateja kuharakisha ufanyaji wa malipo, upokeaji wa mapato na usimamizi wa ukwasi kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Pages