Wachezaji wa timu ya netiboli ya Uchukuzi Sports Club, Grace
Mwasote (kushoto mwenye mpira) akizuiwa na Johari William wakati wa
mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Bandari, Kurasini mwishoni mwa wiki.
Timu hiyo inajiandaa kwa mashindano ya Mei Mosi yatakayofanyika mjini
Dodoma.
Tatu Kitula mmoja wa wafungaji tegemeo akijiandaa kurusha
mpira.
Grace Mwasote akiwa na mpira akiangalia jinsi ya kuwatoka
wachezaji wenzake wa timu ya netiboli ya Uchukuzi Sports Club. Wengine
pichani ni Johari William (kushoto) na Maimuna Ayelo.
Matalena Mhagama mfungaji mkongwe pia wa timu ya Taifa ya netiboli(kushoto), akizuiwa
na Sharifa Mustafa (kulia) huku Mary Kajigili (kushoto nyuma),akiangalia.
Maimuna Ayelo (kushoto) akidaka mpira huku Subira Jumanne
akijiandaa kumzuia katika mazoezi ya timu ya netiboli ya Uchukuzi yaliyofanyika
kwenye uwanja wa Bandari Kurasini, wakijiandaa na mashindano ya Mei Mosi.
Imetolewa na
kitengo cha Sheria na Mahusiano- TAA.
No comments:
Post a Comment