HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 10, 2016

JUMA DUNI HAJI ARUDI CUF

Juma Duni Haji
Aliyekuwa mgombea Mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHEDEMA chini ya Mwamvuli wa UKAWA Juma Duni Haji juzi alirudi katika chama chake cha zamani cha wananchi CUF.

Juma Duni Haji ambae alijiunga na CHADEMA  akitokea CUF mwaka jana katika kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika October 25 mwaka jana kwa makubaliano maalum amechukua kadi ya CUF katika ofisi za chama hicho huko Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja .

Akizungumza katika ofisi ya tawi la Chama hicho huko Kibeni  ambapo alikabidhiwa kadi ya uanachama Juma Duni alisema kuwa alikwenda CHADEMA kwa lengo la kutimiza wajibu pamoja na kujenga heshima ya Chama .


Amesema kuwa wakati yupo CHADEMA aliweza kuisaidia CUF kupata ushindi mkubwa katika ngazi za Ubunge pamoja na udiwani ikilinganishwa na chaguzi zilizopita.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Nassor Ahmed Mazrui alisema kuwa Juma Duni ni kiongozi ambae anajua majukumu yake hususani katika swala zima la haraaka za kisiasa katika kukisaidia chama.

Wafuasi wa chama cha wananchi CUF tawi la Kibeni walifurahishwa na uwamuzi wa aliyekuwa makamo mwenyikiti wa chama hicho Juma Duni Haji kurejea katika chama hicho.

Wakizungumza na Gazeati hili  wananchi hao wamemtaka  Duni Haji kuendelea na msimamo wake wa kudai haki ya wazanzibar katika maswala ya siasa.

Wamesema kuwa kiongozi huyo ambae ni mtendaji katika kusikiliza na kuzifanyia kazi kero za wananchi wake hususani katika kuleta maendeleo ya wananchi walio katika maeneo ya vijijini ambao wanakabiliwa na chanagamoto mbalimbali.

Amesema ushindi wa majimbo uliopata CUF katika uchaguzi wa October 25 ni juhudi zake katika kuhakikisha chama kina simama imara kwa Tanzania kwa ujumla.

Juma Duni Haji ambae mwaka jana alijiunga na CHADEMA chini ya mwamvuli wa UKAWA na Kuwa mgombea mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanznia katika uchaguzi mkuu wa October 25 mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

Pages