HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 25, 2016

MASHINDANO YA RIADHA YA VIJANA CHINI YA MIAKA 19 YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI (EAAR), LIVE ON AZAM TV

MASHINDANO ya riadha ya Vijana chini ya Miaka 19 ya Afrika Mashariki na Kati (EAAR), ambayo yatafanyika Aprili 29 na 30 jijini Dar es Salaam, yanatarajiwa kuoneshwa 'live' Azam TV.
Mashindano hayo yatafanyika Uwanja wa Taifa, huku yakishirikisha nchi tisa huku Tanzania Bara wakiwa wenyeji.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavalla, alisema kwamba wapenzi wa riadha ambao wapo mbali na Dar es Dar es Salaam watafaidika kuona mashindano hayo kupitia televisheni hiyo.

Zavalla, aliupongeza uongozi wa Azam TV kwa kitendo chao cha kiunamichezo ambacho kitachangia kuhamasisha kuendeleza mchezo hapa nchini sambamba na kuitangaza Tanzania kimataifa.

Alisema mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha nchi za Tanzania Bara, Somalia , Djibouti , Kenya , Uganda , Rwanda , Sudan , Ethiopia , Eritrea na Zanzibar.

Alisema mwisho wa nchi kuthibitisha ilikuwa juzi usiku na timu zote tayari zimethibitisha isipokuwa Sudan Kusini.
"Kwa sababu muda umekwisha na hatujapata uthibitisho kutoka Sudan Kusini wala taarifa zozote basi itakuwa imejitoa kwenye mashindano hayo hivyo zimebaki nchi kumi," alisema.

Alisema kwamba wao kama waandaaji, tayari wamekamilisha kila kitu na timu ya Tanzania Bara iko kambini ikiendelea kujifua.

“Timu imeingia kambini wiki iliyopita katika hosteli za Filbert Bayi huko Kibaha, Pwani, ikiwa na jumla ya wachezaji 27 ambao wana afya nzuri na wapo tayari kwa mashindano hayo,” alisema.
 Wanariadhaa wa timu ya taifa ya Vijana chini ya miaka 19 (U-19), wakifanya mazoezi ya viungo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Afrika Mashariki na Kati yanayotarajiwa kuanza Aprili 29-30 kwenye Uwanja wa Taifa. 
 Wanariadhaa wa timu ya taifa ya Vijana chini ya miaka 19 (U-19), wakifanya mazoezi ya viungo.
 Kocha wa timu ya taifa ya Riadha chini ya miaka 19, Robert Kalyahe akitoa maelekezo kwa mwanariadha Rose Seif wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye Uawanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, timu hiyo inajiandaa mashindano ya riadha ya Afrika Mashariki na Kati (EAAR), yanayotarajiwa kuanza Aprili 29-30 Uwanja wa Taifa. (Picha na Francis Dande) 
 Wanariadhaa wa timu ya taifa ya Vijana chini ya miaka 19 (U-19), wakifanya mazoezi ya viungo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Afrika Mashariki na Kati yanayotarajiwa kuanza Aprili 29-30 kwenye Uwanja wa Taifa. 

No comments:

Post a Comment

Pages