NA NEEMA
MWAMPAMBA
MPANGO wa Damu Salama Tanzania (NBTS), umekusanya chupa za damu 43,880 sawa na asilimia 60
ya mahitaji kwa robo mwaka.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Ofisa Mwendeshaji Mpango wa Damu Salama, Abdu Juma alisema katika kipindi cha Robo mwaka benki ya damu huhitaji
chupa 75,000 ili kukidhi mahitaji.
Alisema
licha ya kutofikia mahitaji kiasi kilichopatikana kwa muda huo ni sawa na
asilimia 103 waliyojiwekea ambapo walitarajia kukusanya chupa 42,500.
Juma alisema
katika robo mwaka ya Oktoba hadi Disemba 2015 mpango ulikusanya chupa za damu
11,760 sawa na ongezeko la chupa 32,120 kwa pindi cha Januari-Machi mwaka huu.
“Katika kipindi hiki mikoa iliyoongoza kwa
makusanyo ni Kigoma na Mara ambayo jumla ya chupa 7,580 sawa na asilimia 17 ya
chupa zote zilizokusanywa”alisema Juma.
Pia alisema
licha ya kufanikiwa kwa kiasi hicho bado kuna tatizo la mifuko ya kuhifadhia
damu jambo linalowalazimu wananchi kununua mifuko kwa gharama zao pindi
wanapohitaji kuchangia.
Alitaja
changamoto nyingine kuwa ni mwitikio mdogo wa jamii kuhusu kuchangia damu kwa
hiari kunakopelekea watu wachache kujitokeza kuchangia damu pamoja na
halmashauri nyingi kutotenga bajeti ya kukusanya damu.
Pamoja na
hayo alisema katika robo mwaka ya januari hadi juni na octoba-desemba huwa na
mapungufu makubwa kutokana na wachangaji wakubwa ambao ni wanafunzi na wanavyuo
kuwa likizo.
Hata hivyo
ametoa wito kwa halmashauri zote kutenga bajeti ya kukusanya damu na kununua
vifaa vya kukusanyia damu pia kuhamasisha wananchi kujitokeza kuchangia ili
kuokoa watu wanaopoteza maisha kwa
kukosa damu.
Pia
ameviomba vikundi mbalimbali katika jamii na madhehebu ya dini kushiriki katika
shughuli hiyo kama vikundi vingine vilivyojitokeza na kufanikisha kiasi hicho.
“Nnaomba
watu wajitokeze hali hii inaweza kumkuta mama yako, baba yako, mtoto wako au
ndugu yako yeyote hivyo mjitokeze kuchangia damu tuokoe maisha ya ndugu zetu
wanaofariki kwa upungufu wa damu kila kukicha”alisema Juma.
No comments:
Post a Comment