NA MWANDISHI WETU
BENKI ya NMB imesaini mkataba wa makubaliano baina yake na Mfuko
wa Mikopo ya Matibabu (MCF) kwa ajili ya
kuboresha huduma za afya nchini.
Madhumuni ya mkataba huo ni kuupatia mfuko huo mikopo
mbalimbali ambayo itakuwa inaisimamia kama mdhamini kwa ajili ya hospitali
binafsi, vituo vya afya binafsi, zahanati, watoa huduma za vifaa tiba na vyuo vya
utabibu ili kukuza uwezo kifedha.
NMB inakuwa benki ya kwanza nchini kuingia mkataba na MCF
kwa madhumuni ya kusaidia sekta ya afya.
Aidha, makubaliano hayo yatawezesha watoa huduma za afya
kuwa na uwezo kifedha, ikiwa ni pamoja
na fungu maulumu la usaidizi wa kiufundi
ambalo litasaidia wadau kuchagua watoa vifaa tiba bora na mafunzo kwa matabibu
wao.
Kutokana na uzoefu mkubwa ilionao MCF itakuwa na uwezo wa
kuwadhamini wale wote ambao watakuwa tayari kukopeshwa fedha kwa ajili ya
madhumuni ya kuboresha huduma zao za afya kwa wateja.
Katika makubaliano hayo, hospitali ambazo zitakidhi vigezo
vya kukopeshwa zitakuwa na uwezo
wa kukopa kati ya dola za Marekani 15,000 hadi dola milioni moja ambazo ni sawa na fedha za Tanzania kati ya shilingi milioni 30 hadi
shilingi bilioni mbili.
Akizungumza bada ya
kutiliana saini mkataba huo, Mkurgenzi
Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, alisema
makubaliano hayo yamekuja wakati muafaka, kwa kuwa utawezesha
kuwapo kwa gharama nafuu za huduma za
afya na utajenga uwezo endelevu kwa watoa huduma za afya kuwa na uwezo wa
kuendesha shughuli zao kwa kunufaika na mikopo hiyo.
Naye Mtendaji Mkuu wa MCF, Monique Dolfing-Vogelenzag,
akizungumzia mkataba huo, alisema kuwa ni muhimu kwa ajili ya kutambua kuwa
malengo ya fedha hizo ni kuongeza uwezo
wa utoaji huduma za afya ya msingi nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Ineke Bussemaker (katikati), akibadilishana
hati ya mkataba wa kifedha kwa ajili ya huduma za afya na Ofisa Mtendaji Mkuu
wa Mfuko wa mikopo ya uendeshaji wa hospitali binafsi (MCF), Monique
Dolfing-Volgelenzang katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia
ni Ofisa Mkuu wa Wateja Binafisi, wa NMB, Abdulmajid Nsekela. (Picha na Francis
Dande)
Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Ineke Bussemaker (kulia), akibadilishana
hati ya mkataba wa kifedha kwa ajili ya huduma za afya na Ofisa Mtendaji Mkuu
wa Mfuko wa mikopo ya uendeshaji wa hospitali binafsi (MCF), Monique
Dolfing-Volgelenzang katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia
ni Ofisa Mkuu wa Wateja Binafisi, wa NMB, Abdulmajid Nsekela.
Ofisa Mkuu wa Wateja Binafisi wa NMB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Ineke Bussemaker (katikati), akisaini mkataba wa kifedha kwa ajili ya huduma za afya na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa mikopo ya uendeshaji wa hospitali binafsi (MCF), Monique Dolfing-Volgelenzang katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mkuu wa Wateja Binafisi, wa NMB, Abdulmajid Nsekela.
No comments:
Post a Comment