HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 08, 2016

SERIKALI KUBORESHA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NCHINI

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema serikali ya Tanzania kupitia Ushirikiano wa Kimataifa wa Japani (JICA) imejipanga kuboresha bidhaa zinazozalishwa chini ya kiwango.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar esa salaam, Mwijage alisema serikali imeandaa mpango wa maendeleo wa miaka mitano (FYDP II).

Alisema mfumo huo wa kuwekeza katika biashara kupitia mfumo wa (Kaisen), ambao utasaidia kuboresha viwanda vikubwa na vidogo vilivyopo nchini.

Mwijage alisema mfumo huo utawajengea wafanyabiashara wa viwanda  mazingira mazuri ya kibiashara hivyo wawekezaji wajitokeze.

Alisema mfumo wa ‘Kaizen’ utasaidia kuboresha rasilimali watu, kutengeneza bidhaa zenye viwango vya hali ya juu ambapo tutakuwa tukizalisha kwa tija.

Kwa upande wake mwakilishi wa JICA, Toshio Nagase alisema katika kukuza maendeleo ya viwanda kaizen itasaidia kubadilisha mazingira ya biashara na ushauri katika sera ya viwanda.

Nagase alisema wanasaidia viwanda vidogo kupitia maendeleo,mpango wa dhamana wa mikopo ya SIDO-CRDB,kuendeza viongozi kupitia udhamini wa masomo pamoja na kozi mbalimbali za masomo.

No comments:

Post a Comment

Pages