Msaidizi wa kisheria katika soko la Tabata Muslim, Aisha Juma akizungumza wakati akifungua tamasha la kuongezea uelewa kuhusu kupinga ukatili wa kijinsia masokoni lililofanyika mwishoni mwa wiki Soko la Tabata Muslim jijidi Dar es Salaam ambapo ilielezwa kupungua kwa vitendo vya ukatili katika soko hilo. Upunguaji wa vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia umetokana na elimu iliyotolewa na wasaidizi hao wa kisheria kwa msaada wa Shirika la Equality for Growth (EfG). (Picha na Dotto Mwaibale)
Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la EfG, Mr Shabani akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya ukatili wa kijinsia masokoni.
Wasanii wa Kundi la Machozi lenye maskani yake Temeke jijini Dar es Salaam wakitoa burudani kwenye tamasha hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki viwanja vya Soko la Tabata Muslim.
Burudani zikiendelea katika viwanja hivyo.
Mpiga picha wa EfG akipiga mzigo katika tamasha hilo.
Watoto nao walikuwepo kushuhudia burudani za tamasha hilo.
Katibu wa Soko hilo, John Nombo (kushoto), akichangia jambo kwenye tamasha hilo. Kulia ni Mratibu wa Tamsha hilo,Bibi Grace kutoka Shirika la EfG.
Baunsa wa kujitolea wa Tamasha hilo naye alishindwa kuvumilia midundo ya ngoma iliyokuwa ikitolewa na kundi la Machozi ambapo alijikuta akiingia uwanjani naye kufanya vitu vyake kama anavyoonekana.
Wananchi wakifuatilia tamasha hilo.
Mkazi wa Tabata, Mwahija Rajab akichangia jambo kuhusu ukatili wa kijinsia.
Burudani kutoka kundi la machozi zikiendelea.
Taswira ya jukwaa kuu katika tamasha hilo.
Wageni waalikwa na wasaidizi wa kisheria katika soko hilo na viongozi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment