HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 27, 2016

USAID WAZINDUA MRADI WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA MKOANI MTWARA LEO

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Ally akizungumza wakati wa Uzinduzi wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
 Abdul Kitula ambaye ni mtaalam wa fedha wa mradi wa PS3 akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mradi huo wakati wa uzinduzi hii leo mjini Mtwara.
Mwakilishi wa USAID, Laura Kikuli alikuwepo na kutoa salamu zake katika uzinduzi huo a,mbao ulishirikisha watendaji wa Halamashauri zote za Mkoa wa Mtwara.
 Baadhi ya viongozi wa meza kuu wakifuatilia hotuba za ufunguzi
 Washiriki mbalimbali ambao ni watendaji kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mtwara wakifuatilia mada katika uzinduzi huo.
 Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga akisema neno.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendegu pamoja na wakuu wa Wilaya za Mkoa huo wakifuatilia mawasilisho kutoka kwa maafisa Mradi wa PS3.
 Afisa Rasilimali watu wa  mradi wa PS3, Godfrey Nyombi akitoa mada.
**************
Uzinduzi wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Mtwara  siku ya Jumatano na Alhamisi, Aprili 27-28, 2016.



Mradi huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 97 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji.  Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na  Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha.




Katika uzinduzi huo, mgeni rasmia likuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu. Watu takribani 180 walihudhuria. Washiriki wa uzinduzi huo walikuwani: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Mtwara, Wenye viti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti yaMkoa, na Wajumbe wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye Halmashauri.

 Mkoa wa Mtwara una Halmashauri tisa, ambazoni: Halmashauri ya Mjiwa Nanyamba, Halmashauri ya Mjiwa Newala, Halmashauri ya Wilayaya Newala, Hamashauri ya Mji wa Masasi, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Halmshauri ya Wilaya ya Nanyumbu, Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, na Halmashauri ya Wilaya yaTandahimba.



PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID.  Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni:  Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute. 



Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.



PS3 itaimarisha mifumo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri. Mradi utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania.  Mafanikio yanayotarajiwa ni pamoja na:



·   Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Raia: Uimarishaji wa utawala katika ngazi ya kitaifa na ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, ili kuweza kutumia rasilimali kwa uwazi, kuwezesha ushiriki wa wananchi katika kupanga, kufuatilia, na kutoa matokeo katika kila sekta.



·   Rasilimali Watu: Kuongezeka kwa usawa katika mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utoaji wa huduma bora kwenye maeneo yenye uhitaji zaidi.  Kuimarisha mfumo wa ajira pamoja na kudumu kwa watumishi katika ajira serikalini.



·   Fedha: Ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma, kuongeza ufanisi  katika matumizi ya fedha za umma, na pia kuongeza uwiano kati ya kiasi cha fedha kilichotumika na mali iliyonunuliwa.



·   Mifumo ya Mawasiliano: Kuimarisha mifumo ya utoaji taarifa iliyopo nchini, pamoja na matumizi ya takwimu kwa wadau.



Utafiti Tendaji: Tafiti Tendaji muhimu zitakazosaidia mradi kujua changamoto na mikakati ya kuzishughulikia changamoto hizo. Tafiti hizi zitasaidia kugundua fursa zilizopo na kuzitumia kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa.  Pia tafiti hizo zitasaidia kuboresha maamuzi serikalini.        
 Mtaalam wa Mawasiliano na Takwimu wa Mradi wa PS3, Desideri Wengaa akitoa mada juu ya mawasiliano na utoaji takwimu sahihi.
 Washiriki wakifuatilia kwa makini.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akisisitiza jambo
Wakuu wa Wilaya wakifuatilia mada
 
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akimpa mkono wa shukrani Afisa wa Mradi wa PS3, Abdul Kitula baada ya uzinduzi. Kushoto ni Mwakilishi wa USAID, Laura Kikuli.
 
 Wakuu wa Wilaya wakijadiliana jambo

Picha mbalimbali za makundi tofauti zilipigwa baada ya uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

Pages