HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 27, 2016

WAAMUZI WATAKAOCHEZESHA MASHINDANO YA RIADHA YA VIJANA YA U-19 WAPATA SEMINA

Na Mwandishi Wetu


MKURUGENZI wa mashindano ya riadha ya Vijana chini ya Miaka 19 Afrika Mashariki na Kati (EAAR), Filbart Bayi, amewataka waamuzi wa mashindano hayo kujiamini na kufuata sheria za mchezo huo katika maamuzi yao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika semina ya waamuzi wa mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho, Bayi alisema kuwa wanatakiwa kutoogopa wanapokuwa katika kazi yao.

Alisema kwamba kuna waamuzi ambao wanaogopa watu sura zao na baadaye kuanza kuyumba wanapofanya maamuzi.
"Haya mashindano yanashirikisha nchi tisa, hutakiwi kumuogopa mtu eti kwa kuangalia nchi anayotoka kinachotakiwa ni kujiamini na kufanya kazi yako kiuhakika," alisema.

Alisema kuwa kama muamuzi umesoma  sheria za mchezo na unauhakika na maamuzi yako huna sababu ya kuogopa kwa sababu eti ya lugha anayoongea mchezaji.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kesho na kesho kutwa huku yakishirikisha nchi za Tanzania Bara ambao ndio wenyeji, Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Eritrea, Sudan, Somalia na Zanzibar.

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Omben Zavalla, alisema kwamba tayari timu zimeanza kuwasili nchini ambapo Somalia waliwasili juzi huku nchi za Somalia, Rwanda, Sudan, Ethiopia na Eritrea zimewasili leo.

Alisema kwamba timu zilizobaki zinatarajiwa kutua nchini leo tayari kwa mashindano haya ambayo yatakuwa 'live' Azam TV.


 Mkurugenzi wa Mashindano ya Riadha ya Vijana chini ya miaka 19 (U-19) yatakayozishiriisha nchi za Afrika Mashariki na Kati, Filbert Bayi akitoa mafunzo kwa waamuzi watakaochezesha mashindano hayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Francis Dande)
Baadhi ya washiriki wa semina ya waamuzi wakataochezesha mashindano ya vijana chini ya miaka 19 ya vijana wakiwa katika semina.
Mkurugenzi wa Mashindano ya Riadha ya Vijana chini ya miaka 19 (U-19) yatakayozishiriisha nchi za Afrika Mashariki na Kati, Filbert Bayi akitoa mafunzo kwa waamuzi watakaochezesha mashindano hayo. 
 Baadhi ya washiriki wa semina ya waamuzi.
Meneja wa Mashindano ya Riadha ya Vijana chini ya miaka 19 (U-19), Rehema Killo  akitoa mafunzo kwa waamuzi wa mashindano yatakayofanyika Aprili 29-30 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuzishirikisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. 
Waamuzi wakiwa katika semina hiyo.
Washiriki wa semina hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Riadhaa Mkoa wa Pwani, Joseph Luhende akichangia mada katika mafunzo ya waamuzi watakaochezesha mashindano ya Riadha ya vijana chini ya umri wa miaka 19 kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika Aprili 29-30 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Waamuzi wakiwa mafunzoni.
  Mkurugenzi wa Mashindano ya Riadha ya Vijana chini ya miaka 19 (U-19) yatakayozishirisha nchi za Afrika Mashariki na Kati, Filbert Bayi akitoa mafunzo kwa waamuzi watakaochezesha mashindano hayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. 

No comments:

Post a Comment

Pages