Dar es Salaam, 25, May 2016- Maonesho ya kwanza ya bidhaa za plastiki, mpira, kemikali za petrol na ujenzi yanatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Mlimani City jijini Dare s Salaam kuanzia Mei 27 hadi 29 mwaka huu. Maonesho hayo ambalo yanajulikana kama Africa-PPB-EXPO Tanzania 2016, yatakuwa na washiriki na wageni kutoka nchi zote za Afrika Mashairiki na Kati pamoja na mikutano ya B2B na fursa zinazohusiana.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mkuu wa kampuni ya EXPO ONE ambayo ni waandaji wa maonesho hayo ya EXPO, Ahmed Barakat alisema kwamba maonesho ya Africa-PPB-EXPO yatakuwa ni jukwaa la kipekee la maonesho ya bidhaa mpya na yanatoa mwanya wa kuyaelewa masoko yake ambayo hayafahamiki vizuri.
Africa-PPB-EXPO ni maonesho ya kimataifa ya bidhaa za plastiki, mipira, kemikali za petrol na ujenzi ya nchini Misri.
“Maonesho haya yamebuniwa ni kukuza umoja miongoni mwa Waafrika kwa kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Misri na Tanzania na hali kadhalika kuyaweka masoko yake kwenye ramani ya Afrika,” alisema Barakat na kubainisha kuwa Tanzania ni ya kwanza katika orodha ya nchi za Afrika ambapo Africa-PBB-EXPO imepanga kushirikiana nayo.
Aramex Africa ni mshirika rasmi wa usafirishaji wa Africa-PBB-EXPO na itakwua inatoa mchango mkubwa katika kutoa huduma za ugavi na usafirishaji kutoka Misri hadi Tanzania.
Kupitia Aramex na kwa uratibu wa TanTrade na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Africa-PBB-EXPO inatoa fursa ya kipekee kwa waoneshaji walio na kanzidata za kina kusajiliwa mara zinapopokelewa. Kanzidata hizo zinajumuisha hali ilivyo ndani ya soko la Tanzania na thamani yake pamoja na takwimu sahihi ya kuuza na kuagiza. Hii inatoa fursa ya uhakika kwa mikutano ya mkakati ya B2B pamoja na ufanisi unaohusiana pindi zinapofika.
Meneja Mkuu huyo wa EXPO ONE alitoa wito kwa wafanya biashara kushiriki katika maonesho hayo ili waweze‘kubaini fursa za ushirikiano katika masoko haya mapya pamoja na mtandao ulio na wateja na wenza wa kibiashara.’
“Kwa kushiriki katika maonesho ya Africa-PPB-EXPO, pamoja na mambo mengine washiriki watajifunza jinsi maudhui ya kina ya sekta yanaweza kuathiri biashara zao, umoja uliopo miongoni mwa viongozi wa sekta, kupata washirika wapya na kulinganisha kiwango chao katika mitazamo ya ubunifu.
Kampuni ya EXPO ONE ambayo ni mwandaaji, ni taasisi ya kati ya usimamizi wa mikutano na maonesho ambayo imejikita katika kuandaa na kutoa huduma kwa maonesho ya biashara ya kimataifa pamoja na kuyatangaza mabanda ya Misri katika maonesho ya ndani na ya kimataifa.
Waandaaji wengine ni pamoja na Aramex, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara, Baraza la Mauzo ya Mbolea na Kemikali, Chama cha Wazalishaji na Wauzaji wa Plastiki Misri (Epema) na Taasisi ya sekta Binafsi Tanzania (TPSF). Wengine ni Umoja wa sekta Binafsi Kenya, na Chama cha Biashara Kimataifa China.
Maonesho mengine ya Africa-PPB-EXPO yanatarajiwa kufanyika nchini Senegal na baadaye nchini Angola.
No comments:
Post a Comment