Watoto wakishiriki mbio za Watoto zilizopewa jina la Azania Bank Kids Run 2016 wakianza mbio za Kilometa moja katika viwanja vya Mnaza Mmoja jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Francis Dande)
Askari wa usalama Barabarani akiwa tayari kuongoza mbio hizo.
Washiriki wakitimu mbio.
Washiriki wa mbio za Kilometa 2 wakianza kutimua mbio.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Michezo (BMT), Dioniz Malinzi akizindua
mbio za Kilometa 5 za Azania Bank Kids Run zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mbio za Kilometa 5 wakianza kutimua mbio.
Washiriki wa mbio za Kilometa 5 wakichuana vikali.
Washiriki wa mbio za KM 5.
Mathayo Sima akiwa amewaacha mbali wenzake.
Mathayo Sima akimaliza mbio za Kilometa 5 na kuibuka mshindi wa kwanza.
Mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 5 wavulana, Mathayo Sima akiwa na furaha baada ya kumaliza mbio.
Baadhi ya wazazi wakiwapa watoto wao maelekezo ya mwishomwisho kabla ya kuanza kwa mbio za mita 50.
Watoto wakishiriki mbio za mita 50
Wanariadha wakichuana katika mbio za mita 50.
Watoto wakiwa na wazazi wao kabla ya kuanza mbio za Mita 100.
Watoto wakikimbia mita 50.
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka akizungumza katika mbio hizo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Azania Bank ambao ni wadhamini wakuu wa mbio hizo akizungumza katika mbio hizo.
Mgeni rasmi katika mbio hizo, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo, Dioniz Malinzi akitoa hotuba yake.
Mgeni rasmi akitoa zawadi kwa mshindi wa mbio za mita 100.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT), Dioniz Malinzi akimpongeza mshindi wa kwanza wa mbio za mita 5 za Azania Bank Kids Run, Mathayo Sima.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi (wa tatu kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mbio za Watoto wa Azania Bank Kids Run 2016 akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mbio za kilometa 5 wavulana. Wengine katika picha ni Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka (wa tatu kulia) pamoja na viongozi wa Benki ya Azania ambao ni wadhamini wakuu wa mbio hizo.
Aboubakary Salum akiibusu medali yake.
Mathayo Sima akiwa amewaacha mbali wenzake.
Mathayo Sima akimaliza mbio za Kilometa 5 na kuibuka mshindi wa kwanza.
Mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 5 wavulana, Mathayo Sima akiwa na furaha baada ya kumaliza mbio.
Washiri wa mbio za Kilometa 5 wakimaliza.
Baadhi ya washiriki wakimalizia mbio za Kilometa 5.Baadhi ya wazazi wakiwapa watoto wao maelekezo ya mwishomwisho kabla ya kuanza kwa mbio za mita 50.
Watoto wakishiriki mbio za mita 50
Watoto wakionyesha umahiri wa kukimbia mbio fupi.
Wototo wakichuana.Wanariadha wakichuana katika mbio za mita 50.
Watoto wakiwa na wazazi wao kabla ya kuanza mbio za Mita 100.
Watoto wakikimbia mita 50.
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka akizungumza katika mbio hizo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Azania Bank ambao ni wadhamini wakuu wa mbio hizo akizungumza katika mbio hizo.
Mgeni rasmi katika mbio hizo, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo, Dioniz Malinzi akitoa hotuba yake.
Mgeni rasmi akitoa zawadi kwa mshindi wa mbio za mita 100.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT), Dioniz Malinzi akimpongeza mshindi wa kwanza wa mbio za mita 5 za Azania Bank Kids Run, Mathayo Sima.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Michezo (BMT), Dioniz Malinzi akimvisha medali mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 5, Mathayo Sima.
Mshindi wa kwanza wa mbio za Azania Bank Kids Run 2016 za kilometa 5, Mathayo Sima akipokea zawadi zake kutoka kwa mgeni rasmi.Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi (wa tatu kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mbio za Watoto wa Azania Bank Kids Run 2016 akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mbio za kilometa 5 wavulana. Wengine katika picha ni Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka (wa tatu kulia) pamoja na viongozi wa Benki ya Azania ambao ni wadhamini wakuu wa mbio hizo.
Aboubakary Salum akiibusu medali yake.
Na Mwandishi Wetu
MBIO za Watoto zilizopewa jina la Azania Bank Kids Run 2016, zimefanyika leo jijini Dar es Salaam, ambako Mathayo Sima, aliibuka mshindi katika mbio za kilomita 5 wavulana, akifuatiwa na Antidius Martin.
Katika mbio hizo zilizodhaminiwa na Benki ya Azania, Joshua Paulo alikamata nafasi ya tatu, ambako kwa ushindi huo Mathayo alijishindia medali, fedha taslimu Sh. 200,000, huku Antidius akitwaa medali na Sh. 150,000, wakati mshindi wa tatu Joshua akitwaa medali na sh. 100,000.
Wakali hao pia walijipatia kila mmoja begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo, zawadi ambazo walizipata washindi wa nne hadi wa 10, waliopata pia kifuta jasho cha sh. 15,000.
Washindi wengine na nafasi zao kwenye mabano ni: David Frank (4), Joram Deus (5), Israel Jiro (6), Omary Bawazir (7), Bakari Ali (8), Rahim Seif (9) na Joseph Fabian (10),
Naye George Richard aliibuka kinara wa mbio za kilomita mbili kwa wanaume, akifuatiwa na Florence Lucas, nafasi ya tatu ikichukuliwa na Kassim Khamis. George alijishindia sh. 100,000, huku Florence akijipatia sh. 75,000 na wa tatu ambaye ni Kassim akibeba sh. 50,000.
Hiyo pia ilikuwa ni kategori ambayo pia washindi wa nne hadi wa 10 walijipatia kifuta jasho cha sh. 15,000 na ma begi yenye vifaa vya shule na sare za michezo.
Washindi wa nne hadi wa 10 na nafasi zao kwenye mabano ni: Benjamin Jonathan (4), Edwin Honest (5), Sumeili Letahe (6), Abraham Ali (7), Hamisi Saidi (8), Wilson Daud (9) na Mustapha Hussein (10).
Kwa upande wa wasichana, waliong'ara katika km 2 za Azania Bank Kids Run 2016 ni kinara Regina Deogratius, mshindi wa pili Shadia Ahmad na mshindi wa tatu ni Agness Ernest, ambako Regina alijitwalia medali na fedha kiasi cha shilingi 75,000, Shadia akajishindia medali na pesa sh. 50,000, huku Agness akitwaa medali na sh. 40,000.
Washindi wa mbio za kilomita moja wavulana na nafasi zao kwenye mabano ni: Emmanuel Daud (1), Mecko Hussein (2), Manyama Ephata (3), Awadh Abdulaziz (4) na Ezra Damas (5).
Wengine waliofanya vema kwenye kategori hiyo ni pamoja na Erick Yohana (6), Sebo Hussein (7), Mohamed Ismail (8), Hans Jacob (9) na Deus Pendael (10).
Upande wa wasichana, kilomita moja mshindi alikuwa ni Angela Edwin, mshindi wa pili ni Mariam Jabir, huku mshindi wa tatu akiwa ni Mency Adam.
wengine na nafasi zao kwenye mabano ni: Angel Elman (4), Veronica Adam (5), Feada Manyama (6), Merin Frank (7), Truresha Omary (8), Maria Lohan (9) na Neema Jonas (10).
No comments:
Post a Comment