HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 17, 2016

BILIONI 80 ZATUMIKA KUNUNULIA ZAO LA KARAFUU

Na Mauwa Mohammed Zanzibar

 WAKATI hujuma ya kukatwa kwa mikarafuu ikiongezeka kisiwani Pemba, zaidi ya Tsh. 80.5 bilioni zimetumika na Shirika  la Biashara la Taifa Zanzibar  (ZSTC)kununua zao hilo katika msimu uliopita wa 2015/2016.

Akitoa tathmini ya utekelezaji wa kazi kwa msimu wa vuno la karafuu kwa mwaka 2015/2016, Mkurugenzi Masoka wa ZSTC Salum Abdalla Kibe, katika mkutano na wakulima wa karafuu, madiwani na masheha wa Wilaya ya Micheweni, amesema manunuzi hayo yameweza kuvuka lengo kwa kuzidi tani 245 sawa na (104%) ya makadirio ya mwaka mzima.

Alieleza kwamba msimu huo tani zilizonunuliwa Unguja ni 313 zenye thamani ya shilingi bilioni 4.3 na Pemba tani 5432 zenye thamani ya shilingi bilioni 76.2, huku tani zilizokadiriwa kununuliwa na shirika hilo kwa msimu huo ni 5,500 ambapo Unguja tani 217 na Pemba tani 5283.

 Aliwapongeza wakulima wa karafuu kisiwani Pemba kwa juhudi zao za kuuza karafuu zao katika shirika la ZSTC, ambapo makisio ya awali yalikuwa ni Tani 3,200 kwama msimu huu.

 Akizungumzia changamoto zilizojitokeza msimu uliopita amesema bado baadhi ya wakulima wanawasilisha karafuu zilizochanganywa na makonyo, matende, kutoku kauka ipasavyo na zinakuwa na uchafu  usiotakiwa.   

Changamoto nyengine ni Uanikaji wa karafuu hauzingatii maelekezo ya kuimarisha viwango vya ubora, kwani huanikwa barabarari, kwenye paa au sakafuni, Baadhi ya wakulima  huhifadhi karafuu zao katika vipolo baada tu ya kukauka na kupeleka karafuu zao vituoni bila kujua asili ya kipolo wenyewe kilikua kimebeba nini.

Alisema Fedha zinazokopeshwa kwa wakulima, baadhi yao hawarejeshi kwa wakati, na wasio waaminifu hawarejeshi kabisa hivyo kusababisha Shirika kuingia gharama za ziada katika kufuatilia madeni, Kuendelea kulipa fedha taslimu vituoni kwa kiwango kikubwa mfano kinachozidi milioni mbili na nusu ambapo inaweza kuhatarisha usalama wa mkulima.

Alifahamisha licha usafirishaji wa karafuu kwa magendo umepungua, ila bado kuna baadhi ya wafanyabiashara ya karafuu hushirikiana na wananchi wasio waaminifu na kufanya biashara ya magendo ya karafuu.

Mapema akifungua mkutano huo wa wakulima Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Pemba, Omar Khamis Othamna, aliwataka wakulima wa wilaya ya Micheweni kuhakikisha wanalipa madeni wanayodaiwa na ZSTC baada ya kukopeshwa pesa hizo na shirika.

Alisema shirika limekuwa na utaratibu mzuri wa kuwakopesha wakulima wake, ambapo jumla ya shilingi Milioni 47,000,000/= zimekopeshwa na Milioni 32,000,000/= zimerudishwa huku Milioni 14,000,000/= bado ziko mikonini mwa wakulima.
Alisema shirika limekuwa na limeanzisha utaratibu mzuri wa kuhakikisha linawakopesha wakulima wake, ili kuweza kuwasaidia pale wanapopata na matatizo.
Hata hivyo aliwatakla wakulima kuhakikisha wanahifadhi karafuu zao vizuri, pamoja na kuacha tabia ya kuzichanganya na uchafua ambao unapelekea karafuu za Zanzibar kuanza kushuka bei.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi wa ZSTC, Maalim Suleman Kassim, alisema zao la karafuu ni muhimu sana kwa Zanzibar, kwani ndio utu wa mgongo wa taifa, hivyo wakulima wanapaswa kulithamini sana kwa kuacha kulifanyia udanganyifu.

Alisema wananchi wengi wa Unguja na Pemba wamekuwa wakitegemea zao hilo, hivyo haipenzi sasa kulianza kuliharibu kwa kufanya udanganyifu.
Naye afisa mdhamini wa shirika la ZSTC, Abdalla Ali Ussi alsiema ZSTC imekuwa na utaratibu wa kukutana na wakulima kila Mwisho wa msimu kwa lengo la kuwashukurua juu ya juitihada zao za kuuza zao katika ZSTC.
Aidha alisema dunia nzima karafuu chafu ni karafuu za Zanzibar, hivyo wakulima munapasw akuhakikisha munazisafisha karafuu zenu kabla ya kuzipeleka shirika.

Alifahamisha kuwa licha ya kuchangwanywa hivyo, lakini bado ladha ya karafuu ya Zanzibar iko pale pale, huku akiwataka wakulima wa micheweni kuhakikisha wanarudisha fedha walizokopeshwa na ZSTC.

No comments:

Post a Comment

Pages