HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2016

Hatuna ugovi na Serikali ya Muungano

Na Talib Ussi na Mauwa Muhammed
 
 Chama cha wananchi CUF kimesema kuwa wao hawana ugomvi na serikali ya Muungano ugomvi wao ni serikali ya Mapinduzi  Zanzibar (SMZ) kwa madai kuwa imepora maamuzi ya wananchi katika uchaguzi uliofanyika October mwaka jana.

Kauli hiyo  ilitolewa na aliyekuwa katibu Mkuu wa chama hicho  Maalim Seif Sharif Hamad  wakati akizungumza na viongozi wa wilaya ya Magharibi A na B  huko katika ofisi ya chama Kilimahewa Mjini Zanzibar.

Alisema ziadi ya 80% ya wananchi wa Zanzibar waliikataa CCM na viongozi wake na kudai hawawezi kukubali hata siku moja kuongozwa na utawala wa mabavu.

“mkakati wetu tutahakikisha hatumwagi tone la damu lakini  Dk shein ataondoka marahii”alisema maalim Seif.

Maalim Seif ambae ni makamo wa kwanza mstaafu alisema  Wazanzibari wana jukumu la  kumuondosha Dk Shein  kutokana na kukosa ridhaa ya walio wengi.

Hata hivyo alisema ajenda yao kubwa ni kuhakikisha wanaiondoa serikali ya Dk Shein kwani katiba zote ile ya Muungano na ya Zanzibar inasema njia ya kuweka uongozi  ni kupitia  uchaguzi ulio huru na wa haki.

“Sisi tunasema tutafanya harakati zetu mpaka shein aondoke na wala wasidhani tutapigana”Alisema  Maalim  Seif.

 Katika kikao hicho Mkurugenzi wa mipango na chaguzi wa chama hicho Omar Ali Shehe alisema ziara aliyoifanya katibu mkuu wa chama chake imeonyesha wanachi wanataka serikali yao ya halali ambayo waliipigia kura October mwaka jana.
 
Aidha Shehe alisema baada ya chama cha Mapinduzi kushindwa kufanya siasa wanatumia njia ya kukidhalilisha chama chake ili kisiweze kufanya shughuli zake za kisiasa.

Nae mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama hicho salim Abbdlla Bimani amelishutumu Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa kuzuwia  mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyike Juni  2 maka huu.

Alisema mkutano huo umezuwiwa   kwa madai ya kuwepo kwa ugeni kutoka ndani na nje ya nchi wanaokuja katika Ijitmai ya Kimataifa.

Alisema licha ya RPC wa mkoa Kaskazini Hasina kuwataka kutoa tarifa ya maombi wakati wanapohitaji kufanya mikutano wa hadhara.

“tuna uthibitishia ulimwengu kuwa jeshi la polisi limendelea na kukandamiza demokrasia na linatumika kisiasa “alisema Bimani.

Alisema kwa mujibu wa barua waliyoipokea kutoka jeshi la polisi iliyotiwa saini na SP Ali Haji mkuu jeshi la polisi Wilaya ya Kaskazini B imekitaka chacha CUF kusitisha mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika Juni 2 mwaka huu.

Tarifa hiyo imesema kutokana na shughuli mbali mbali kutoka nje ya nchi kwa ajili ya ijitmai shughuli hizo kama zilivyo shughuli nyengine zenye kujumuisha mikusanyiko mikubwa hulazimisha jeshi hilo la polisi kuwa katika utendaji wa kazi zaidi ya wakati za kuhakikisha kunakuwepo amani na usalama.

Mkutano huo wa wilaya za magharibi A na B ni  wa mwisho katika ziara za Katibu Mkuu kichama za kutembelea Wilaya za Unguja na Pemba zilizoanza Mey 14 hadi 18 kwa kisiwa cha Pemba na  Mey 28 hadi Juni 2 katika kisiwa cha Unguja.

No comments:

Post a Comment

Pages