Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jamine Tisekwa akiungana na kwaya ya Kikundi cha Sanaa za Maonesho cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakati burudani ikitolewa bure kwa wananchi katika Bustani ya Nyerere Square mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Sanaa JWTZ ilitoa pia burudani za sarakasi, taarabu, ngoma za asili, Steel Band na muziki wa bendi ya Mwenge Wana Paselepa
Burudani hiyo ilikonga nyoyo za wananchi waliofurika kushuhudia ambapo hata muda wa kumaliza ulipowadia hawakutaka watoke eneo hilo.
Akizungumza Mkuu wa Wilaya kuhusu onesho hilo, alisema kuwa ni jambo ambalo hawakulitegemea hivyo wanaomba tena Sanaa JWTZ wapange siku nyingine waburudishe kuanzia mapema saa nane hadi jioni ili wananchi wa mkoa huo wafarijike vya kutosha.
Baada ya kumalizi hapo kundi hilo la Sanaa Jwtz lilikwenda kutumbiza usiki kwenye Chuo cha Mipango Dodoma.
Akizungumza Msemaji wa JWTZ SANAA, Hope Dagaa alisema hivi sasa kikundi chao wamekiboresha na kwamba hivi sasa wanataka warudi kwa nguvu zote kwenye kumbi kutoa burudani murwa kwa wananchi, kama ilivyo kuwa zamani. HABARI,PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mkuu wa Wilaya akicheza pia ngoma ya kibati ya asili ya Zanzibar.
Ngoma ya kibati.
Mwenge Jazz ikifanya vitu vyake.
Wananchi wakishuhudia.
Steel Band ikitumbuiza.
Umati wa wananchi wa Dodoma wakifarijika na burudani murwa iliyokuwa ikitolewa hapo
Ngoma ya kibati ikichukua nafasi yake
Mkuu wa Wilaya akiwatuza wasanii
Msemaji wa Sanaa JWTZ, Hope Dagaa akiwa na Mkuu wa Wilaya Tisekwa
Mkuu wa Wilaya akicheza wakati kwaya ikitumbuiza
Mkuu wa Wilaya, Tisekwa akiwa na wasanii wa JWTZ
Kikundi cha Kwaya
Steel Band
Band ya Mwenge Jazz
Taarab na Sarakasi.
No comments:
Post a Comment