1. Waamuzi wa mechi za Jumapili
2. Msimamo wa TFF kuhusu Stand United
3. Waamuzi mchezo wa Young Africans v TP Mazembe
Waamuzi
wanne kutoka Ethiopia, ndio watakaochezesha mchezo wa kimataifa kati ya
timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti
Boys’ na Shelisheli utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo
huo ni wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa
vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Waamuzi hao ni Belay Tadesse
Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw
Belachew upande wa kulia na Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku
mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma Nigussie. Kamishna wa mchezo huo atakuwa
ni Bester Kalombo.
Serengeti
Boys ilikuwa kambini tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa
kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa
Shelisheli utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa,
jijini Dar es Salaam. Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na
Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.
Katika
kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako
walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA
(AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya
kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Kadhalika
Serengeti Boys ilicheza mfululizo michezo saba ya kimataifa bila
kufungwa dhidi ya Misri (2), India, Korea Kusini, Malaysia na Marekani
(USA). Kabla ya hapo timu hiyo ilicheza michezo kadhaa ya ndani na timu
za chini ya umri wa miaka 20 bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Katika
mashindano ya AIFF, timu hiyo pekee kutoka Afrika na ambayo ilikua
kipenzi cha mashabiki katika jiji la Goha ilicheza na timu ambazo ziko
juu katika hatua za juu katika mtoano wa kuwania kushiriki Kombe la
Dunia kupitia mabara yao yaani CONCACAF (USA) na AFC (India, Korea na
Malaysia).
Awali
timu ya Serengeti Boys ilipewa nafasi ndogo ya kufanya vizuri kwa
sababu ya rekodi zilizokuwa zinaiweka Tanzania katika viwango vya chini
katika umri huo kwa nchi za Afrika Magharibi na Kaskazini zilikuwa juu
zaidi na vilevile ukweli wa kwamba timu kama USA, Korea, Malasyia na
India zilikuwa na bajeti kubwa iliyogharamiwa na Serikali zao na
walikuwa na vifaa vya kila namna kiasi cha kuomba magari kwa ajili ya
vifaa vya mazoezi na mechi.
Serengeti
Boys ilimaliza Mashindano ya AIFF katika nafasi ya tatu kwa kuifunga
Malaysia mabao 3-0. Serengeti Boys na Bingwa Korea hawakupoteza mchezo
hata mmoja na awali walipokutana walitoka sare ya 2-2.
MWAMUZI WA ANGOLA KUWAAMUA YOUNG AFRICANS, TP MAZEMBE
Mchezo
wa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Young Africans ya
Dar es Salaam, Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC), utachezeshwa na Mwamuzi Janny Sikazwe wa Zambia.
Sikazwe
atasaidiwa na Jarson Emiliano dos Santos kutoka Angola atayekuwa kwenye
mstari wa kulia (line 1) na Berhe O’Michael wa Eritrea atayekuwa upande
wa kushoto (line 2) huku Wellington Kaoma wa Zambia akiwa ni mwamuzi wa
akiba. Kamishna wa mchezo huo atakuwa Celestin Ntangungira wa Rwanda.
Pia mchezo huo utakuwa na Mratibu Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio
Jose Mugadza.
SUALA LA STAND UNITED YA SHINYANGA
Kutokana
na mkanganyiko wa uendeshaji wa mchakato wa uchaguzi katika Klabu ya
Stand United ya Shinyanga, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF),
limeagiza michakato yote miwili inayoendeshwa sambamba ndani ya klabu ya
Stand United, isimamishwe mara moja kisha kusubiri maelekezo mengine.
No comments:
Post a Comment