Na Talib Ussi, Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewata wastaafu kuacha kuomba omba na badala na badala yake wabuni miradi ya kuwaendeleza katika maisha yao ya uzeeni.
Alieleza kuwa baadhi ya watumishi hao wana uwezo kamili wa kiafya ambao unawapa uwezo wa kufanyakazi lakini wanashindwa kubuni na badala yake wanaingia katika tabia ya kuomba.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akizungumza na Uongozi wa Jumuiya ya Wastaafu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wanaoishi Zanzibar walipofika Ofisini kwake Vuga Mjini wa Zanzibar.
“Baadhi ya Watumishi wa Taasisi za Umma bado wana hofu ya kustaafu utumishi wao wakihisi kunyemelewa na ukali wa maisha ya baadaye huku mnasahau kwamba maisha baada ya kustaafu yapo kama kawaida” alieleza Balozi Seif.
Alisema cha msingi kwa mtumishi anayehusika ni kujipanga mapema katika kujiandaa na harakati za kujiendesha kimaisha bila ya kutetereka mara amalizapo utumishi wake.
Mapema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wastaafu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mohammed Ali alisema mawazo waliyopewa na kiongozi huyo watayafanyiakazi ili kuhakikisha Wastaafu wanajikwamua kimaisha.
Alieleza kuwa watafanya wanaloliweza kuhakikisha wanachama wao wanakuwa na miradi ya kujikwamua katika maisha yao ya kusataafu.
No comments:
Post a Comment