Mwenyekiti
wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiongozana na Makamu
Mwenyekiti cha Chadema, Zanzibar, Said Issa Mohamed wakiwasili katika mkutano
na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, leo,
wakati wa kutoa tamko la kuahirishwa kwa maandamano ya UKUTA. (Picha na
Francis Dande)
Waziri Mkuu
wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa akiwasili katika
mkutano huo. Kushoto ni Mbunge wa Kibamba, John Mnyika.
Viongozi wa
Chadema wakiwa wameshikana mikono kuonyesha mshiokamano wao wakati wa mkutano
na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es salaam, leo
wakati wakitoa tamko la kuahairishwa kwa maandamano ya UKUTA.
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisisitiza jambo
wakati wa mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar
es Salaam.
Waziri Mkuu
wa zamani, Edward lowassa akipeana mkono na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe. Katikati ni Said Issa Mohamed ambaye ni Makamu Mwenyekiti Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe akipeana mkono na mbunge wa Kibamba, John Mnyika.
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akizungumza na
waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho.
Waziri
Mkuu wa zamani, Edward lowassa ambaye pia na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,
Edward Lowassa akizungumza katika mkutano huo.
Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo ametoa maadhimio ya Kamati Kuu ya chama
hicho (CC), kuhusu kuahirishwa kwa uzinduzi wa Maandamano ya UKUTA hadi Oktoba
Mosi ili kutoa nafasi kwa viongozi wa dini ili kukutana na Rais Dk. John
Magufuli kwa maslahi ya Taifa.
Akitoa
tamko la maamuzi ya Kikao cha Kamati Kuu (CC), mbele ya waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema kuwa
sababu kubwa zilizofanya kuahirisha kwa maandamano hayo ni kutoa nafasi kwa
viongozi wa dini waliotaka kuahirishwa kwa uzinduzi wa maandamano hayo ili
kutoa nafasi ya mazungumzo ya viongozi wa taasisi mbalimbali za dini na Rais
John Magufuli.
Katika
mkutano huo Mbowe alisema kuwa walikutana na taasisi za dini zikiwemo Baraza la
Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Makanisa ya Kipentekoste ya Karismatiki,
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na Mufti Mkuu wa Zanzibar, Baraza la
Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) na Kanisa la African Inland
Church Tanzania (AICT).
Pia walikutana na taasisi za kiraia kama Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Jukwaa la Wahariri (TEF), pamoja na Jukwaa la Katiba (JUKATA).
No comments:
Post a Comment