Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei leo Septemba Mosi amefanya ziara katika baadhi ya matawi ya Benki hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam kujionea utendaji kazi na kukabiliana na changamoto zilizopo.
Katika ziara hiyo pamoja na kukagua utendaji kazi, Dk. Kimei pia alitumia fursa hiyo kukutana na kuzungumza na wateja.
Dk. Kimei pia alitembelea ATM za Benki hiyo zilipozo maeneo ya Namanga-Msasani, Mikocheni, Tegeta, Mbezi na Millennium Tower na kuahidi kuwa Benki hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa huduma hiyo inaendelea kuboreshwa ili kufikia mahitaji ya wateja. "Hivi sasa tuna zaidi ya ATMs 400 na tunajipanga kufikisha ATM 500 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Pia aliongeza kuwa "Tumeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa ATM zetu zinajazwa pesa kwa wakati ili kuondoa usumbufu wowote kwa wateja wetu" alisema Dk. Kimei.
Kutoa fedha katika ATM ya Millennium Tower.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhcm1Thjl6hXOtCQXpWj3_H9DUokw3mdIYqyDPsfZS_dHV8bJijQ3VszG3NCUqHyecM2OxQW66i53EExx7Z1-8uqy1hb42ftxbpxwfWDgu2kHht8htk33TOLutu1JMzB8ub9m_-6DRl63f6/s640/_MG_3492.JPG)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo kwa waandishi wa habari baada ya kufanya ziara katika baadhi ya matawi ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo kwa waandishi wa habari baada ya kufanya ziara katika baadhi ya matawi ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment