NA KENNETH NGELESI, MBEYA
MCHEZO wa fainali kombe la Kimondo Cup 2016 kati ya Maji Fc dhidi ya Yoso FC zote kutoka Mbozi Mkoani Songwe ulivunjia dk 34 baada ya mashabiki kuvamiwa uwanja wakati huo Yoso FC walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0 lilifungwa na Akida Mwasyika Dk. 32 ya mchezo.
Mchezo huo wa fainali Kombe la Kimondo Cup 2016 ulichezwa Semptemba 18 mwaka huu katika wa Shule ya Msingi Mlangali na kushudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palyango, mashabiki wa timu zote mbili walianza kupigana kwa kurushia chupa bia virungu vurungu na kusambaa uwanja wote hali iliyomfanya mwamuzi wa mchezo huo John Njavike kushindwa kuendelea kutokana hali ya usalama kutoweka.
Akizungumza na Tanzania Daima,Mwasenga shuhuda wa mchezo huo alisema kuwa chanjo,cha vurugu hizo ni baada ya mashabiki wanaodaiwa kuwa ni wa timu ya Maji Fc kumrushia shilingi 1000/ golikipa wa timu Yoso ili achie goli na kama hata tekeleza hivyo mpira usingendelea.
Baada ya hali hiyo kutokea mashabiki wa Yoso fc walikuja juu ya kuanza kupigana hali iliyofanya mwamuzi kushindwa kumudu mchezo na hatimaye kuaarisha.
Akizungumza mara vaada ya kuahirisha mchezo huo Mwamuzi Njavivike alisema hali ya mchezo ulikuwa nzuri tatizo ni vurugu za mashabiki ambao wametofautiana kauli nje ya uwanja na hatimaye kuingia uwanjani na mchezo umeshindwa kuendelea.
‘Mchezo ulikuwa mzuri lakini tatizo ni vurugu zilizo anzishwa mashabiki kwa mashabiki na kama unavyoona hali ya usalama siyo nzuri hakuna ulinzi wowote hivyo tumeona vyema kuahisha mchezo tutasubiri waandaji wa mashindano hao wataaongea nini?’ alisema Njavike
Kabla ya mchezo huo kulikuwa na mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu na wanne ambapo timu ya Makua FC ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 baada ya kuishikisha adapo timu ya Ikupa bao la Makua FC lilifungwa na Brain dk 17 ya mchezo.
Naye Erick Ambakisye muandaaji wa mashindano hayo alisema kuwa wameamua kuvunja mchezo huo sababu za kiusalamu kuto kuwa nzuri na kwamba mchezo huo wa fainali utapigwa katika Uwanja wa CCM Vwawa.
Alisema kuwa dalili za mchezo huo kuvunjika zilionekana kwani kabla ya pambalo kuanza mashabiiki wa timu zote mbili walikuwa wakitambiana kuwa endepo moja itaanza kupata goli basi mchezo huo usingeweza kuendelea na hicho ndicho kilichotokea kwa dk 2 tu baada ya Yosa kupta bao vurugu zilianza hali hiyo imeasasabibnisha mchezo kuahishwa.
Katika hatuA nyingine Ambakisye alibainisha zawadi kuwa Bingwa wa mashindano hayo atajinyakulia kitita cha shilingi laki tano (500,000) na mpira mmoja, wakati mshindi wa pili ataondoka na laki tatu (300,000) na mpira mmoja huku mshindi wa tatu Makau fc atajishindia kiasi cha shilingi laki mbili (200,000) na mpira mmoja,wakati atakaye shika nafasi ya nne ataondoka na mpira
Mashindano ya Kimondo CUP ayameashisiwa na Ambakisye diwani wa kata ya Mlangali na Mwenye wa Halmashuri ya Mbozi Mwaka 2011 yakiwa na lengo la kukitangza Kimondo kilichoto katika kata hiyo ya Mlangali.
No comments:
Post a Comment