HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 20, 2016

JESHI LA POLISI KILIMANJARO LAWATUNUKU ZAWADI ASAKARI WAKE 34

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akipokea salamu za heshima kutoka kwa askari wakati wa gwaride maalum lililoandaliwa wakati wa hafla fupi ya kutunuku zawadi kwa askari 34 wa vyeo mbalimbali waliotekeleza vyema majukumu yao. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akikagua gwaride la heshima baada ya kuwasili katika viwanja vya kikosi cha kutuliza ghasia mjini Moshi kwa ajili ya hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 waliotekeleza vyema majukumu yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa askari 34  waliotekeleza vyema majukumu yao.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiq akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 waliotekeleza vyema majukumu yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akimuoneesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq baadhi ya silaha zilizokamatwa hivi karibuni zikidaiwa kutumika katika vitendo vya uharifu.
Mkuu wa Kitengo cha dawa za kulevya cha jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Mkaguzi wa Polisi,Ezekiel Midala akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro sehemu ya dawa za kulevya zilizokamatwa na jeshi hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akitunuku zawadi kwa baadhi ya askari waliofanya vizuri katika kutekeleza majukumu yao.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Pages