HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 17, 2016

MKUU WA WILAYA YA ILALA AONGOZA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUCHANGIA MAAFA YA TETEMEKO BUKOBA

1
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akipokea kiasi cha shilingi milioni zaidi ya milioni 6 kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa Kariakoo Bw. Deo Senya wakati Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK) walipofanya Harambee ya kuchangia wahanga wa Tetemeko la Ardhi kule Bukoba mkoani Kagera ambapo Mkuu wa wilaya hiyo aliongoza harambee hiyo, Kuliani ni Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala Bw. Edward Mpogolo na katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanya Biashara Kariakoo Bw.Philimin Lomano Chonde.

Katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 13,708,000/= fedha taslimu zilikusanywa na vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 31564800/= jumla ya michango kwa ujumla ni shilingi milioni 45,672,800/= harambee hiyo leo ilikuwa inazinduliwa rasmi na michango inaendelea mpaka siku ya jumamosi ijayo ambapo ndiyo harambee hiyo itafungwa rasmi na wafanyabiashara mbalimbali wametakiwakuendelea kuchangia kwa kupitia jumuiya yao ya wafanyabiashara mpaka siku ya jumamosi.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Mh. Sophia Mjema akipokea msaada wa viatu kutoka kwa wafanyabiashara wa kikundi cha Raha Square.
3
Raha Square Kariakoo wakikabidhi mchahgo wa fedha.
6
Wakikabidhi Suti na vitengi pamoja na mashuka katika harambee hiyo.
7
Mkuu wa wilaya ya Ilala akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo mara baada ya harambee hiyo.
9
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akiwahutubia wafanyabiashara na wananchi mbalimbali waliohudhuria katika harambee hiyo.
10
Mfanyabiashara Mohammed Abdallah Nofa akizungumza mara baada ya kukabidhi mchango wake wa shilingi 500.000 kwa Mkuu wa wilaya Ilala Mh. Sophia Mjema wa pili kutoka kulia . katika picha kulia ni Edward Mpogolo Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala na Kushoto ni Katibu wa JWK Bw. Abdallah Mwinyi.
12
Kiongozi wa Wafanyabiashara wauza Simu za mkononi Bw.Stanley Mwakipesile akizungumza machache mara baada ya kukabidhi mchango wao zaidi shilingi milioni 1.500.000 kwa mkuu wa wilaya ya Ilala katika Harambee hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages