Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akizungumza katika Bonanza la 11 la Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha. |
Na Mwandishi Wetu
Arusha. Timu
ya soka ya waandishi wa Habari za
michezo nchini, (Taswa FC) na netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo
nchini, Taswa FC Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC)
zimetwaa ubingwa wa bonanza la 11 la Waandishi wa Habari la Arusha.
Taswa FC na Taswa Queens ambazo zinadhaminiwa na
kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia na Benki ya Posta Tanzania (TPB)
zilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika bonanza hilo la kusisimua na
waandishi kushindana katika michezo mbalimbali mbali ya soka na netiboli.
Timu ya
Wazee Club ambao ilishika nafasi ya pili, ndiyo pekee iliyonusurika na kichapo
katika bonanza hilo aada ya kuambulia
sare ya mabao 2-2. Hata hivyo, timu hiyo ilibidi ifanya kazi ya ziada baada ya
kusawazisha mabao mawili katika dakika sita za mwisho.
Timu ya Chuo
cha Uandishi wa Habari na Utangazaji cha
AJTC kilishika nafasi ya tatu na timu ya mwisho ni Redio Sunrise.
Taswa FC
ilianza kwa kasi na kufunga mabao mawili
ya haraka haraka kupitia kwa Saidi
Seifu akipokea pasi safi za Majuto “Dr Regret”
Omary. Martin Shila, Edrward Mbaga, Muhidin Sufiani, Zahoro Mlanzi,
Salum Jaba na kipa wao, Mwarami Seifu walikuwa kizingiti kikubwa katika mechi
zote.
Katika mechi
ya pili, Taswa FC ilishinda mabao 4-0n dhidi ya Sunriseb Redio , bao la kwanza
likifungwa na kapteni, Wilbert Molandi kwa kuunganisha kona ya Hare Temba na
baadaye Saidi Seifu akifunga mabao matatu kufutia pasi ya Athumani Jabir na
Majuto Omary ambaye alitoa pasi ya bao la tatu na la nne.
Katika
mchezo wa mwisho, Taswa FC iliibuka na ushindi wa ba 1-0 dhidi ya AJTC, bao la
dakika za majeruhi lilifungwa na Ali “Maradona” Salum kufuatia kona safi ya
Majuto.
Timu ya
netiboli ya Taswa Queens ilifanya ‘mauaji’ kufuatia ushindi wa mabao 30-2 dhidi
ya AJTC. Mabao ya Taswa Queens yalifungwa na Sharifa Mustapha aliyefunga mabao
22 na Rose Michael aliyefunga mabao nane.
Taswa Queens
ilitawala sana mchezo huo kupitiaa wachezajia wake, Zuhura Abdinoor, Johari
William, Elizabeth Mbasa, Tatu, Mage na Vicky Godfrey.
Timu zote
hizo zilizawadiwa kitita cha sh 100,000 kila moja na kombe. Kwa upande wa kukimbiza Kuku, Taswa Queens
pia walifanikiwa kuibuka na ushindi wakifuatiwa na Sunrise Radio ambao wote
waliondoka na kuku kila mmoja.
Mgeni rasmi
katika bonanza hilo la 11 lillilofanyika katika viwanja vya General Tyre
alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro ambaye alisema kuwa
waandishi wa habari ni muhimu kushiriki michezo ya aina mbalimbali ili kuiweka
miili vizuri.
No comments:
Post a Comment