HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 12, 2016

MAALIM SEIF AWATAKA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI

Na Talib Ussi, Zanzibar

Makamu wa Kwanza mstaafu, Maalim Seif Sharif Hamad amendelea kuwaomba Watanzania  kudumisha amani hasa katika kipindi hichi Skukuu na kuwaomba kuwaombea dua wazao waliopata maafa ya tetemeko la Ardhi huko mkoa wa Kagera.

Maalim Seif aliyaeleza hayo Kiemba Samaki Zanzibar   mara baada ya swala ya IDD Al Hajji kumalizika.

Alisema kila mmoja anaelewa mitihani iliyowapata wananchi wa Bukoba na maeneo mengine na kuwata wananchi kutumia sikukuu hii kuwaombea kwa mola wao na wao wapate faraja.

“sisi tunasheherekea skukuu hii katika hali hii lakini wezentu wemepata mtihani mkubwa ambao umepeleka watu kadhaa kupoteza maisha” alieleza Maalim Seif.

Alitumia fursa hiyo kuwata wananchi wote waliuopata maafa hayo kuwa na subra kutoka na mtihani huo mzito.
Sambamba na hilo alieleza kuwa sikukuu inamaelekezo yake na kueleza kuwa ni vyema kuyafuata na kuaza kuwaona wale waliopatwa na maafa hayo kuwasaidia kwa kulingana na uwezo.

Alisema vitabu vya dini zoote zimeelekeza kuwa binaadamu waishi kama kiwiliwili, ili mwezao anapopata mtihani wahisi kama umepata yeye.

Aidha Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF alitumia muda huo kutoa mkono wa Iddi kwa watanzania woote na kuwatakia sherehe hizo kwa mujibu wa miongozo ya Dini ya kiislamu.

Juzi Mkoa wa Kagera na maeneo jirani yalipata mtihani mzito wa tetemeko la Ardhi na kupelekea watu 15 kufariki na wengine 100 kuwa majeruhi.

Wakati Maalim Seif akiyaeleza hayo Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Muhammed Shein amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuitumia vyema skukuu hii ili kudfumisha umoja miongoni mwa Waislamu.

Alieleza kuwa tofauti za kisiasa zisiwe chanzo cha kuwepo mivutano baaina ya viongozi wa kidini alidai kufanya hivyo ni kinyuume na maarisho ya Allah.

Aliwataka wazanzibar kusheherekea Skukuu hiyo kwa kutembeleana na kuwatakia dua wazee ambao tayari wametangulia mbele ya haki.

No comments:

Post a Comment

Pages