Meneja
Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, (kulia), akiwasaidia
wanakijiji hawa wa Ikwiriri, Wilayani Rufiji mkoani Pwani, kutuma michango kwa
njia ya mtandao wa simu, wakati wa kuandikisha wanachama chini ya mpango wa
Wote Scheme kwenye chuo cha Maendeleo ya Jamii, Ikwiriri, Oktoba 3, 2016. Takriban wanakijiji 395
wakiwemo, wakulima, wafuga nyuki, wavuvi na waendesha bodaboda, wamekabidhiwa
kadi za uanachama kupitia mpango huo unaoruhusu mtu yeyote aliye kwenye sekta
rasmi na isiyo rasmi kujiunga kwa kuchangia kila mwezi kima cha chini shilingi
20,000.
Meneja
wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya, (kulia), akimkabidhi kadi ya
uanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari, (Wote Scheme),
wakati wa kuandikisha wanachama na kugawa kadi kwenye viwanja vya chuo cha
ufundi Ikwiriri, wilayani Rufiji mkoa wa Pwani, Oktoba 3, 2016.
Zawadi Hamza Sule, (kushoto), ambaye ni mkulima huko Ikwiriri, akipokea kadi yake ya uanachama wa PPF kupitia Wote Scheme
NA
MWANDISHI WETU, IKWIRIRI
MFUKO
wa Pensheni wa PPF, kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari, “Wote Scheme”,
umesajili karibu wanachama 400 huko
Ikwiriri wilayani Rufiji mkoa wa Pwani.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa zoezi la usajili na ugawaji kadi za uanachama
kwenye viwanja vya chuo cha Ufundi Ikwiriri, (IFDC), Oktoba 3, 2016, Meneja wa
PPF Kanda ya Temeke, Erica Meshack Sendegeya, alisema, wanakijiji hao wajasiriamali walihamasika
kujiunga na mpango huo baada ya Kanda yake kutoa elimu juu ya umuhimu wa
wananchi kujiunga na Mfuko huo kwani kuna manufaa mengi.
“Tuliwaeleza,
mpango huu wa Wote Scheme umebuniwa ili kutoa fursa ya wananchi walioajiriwa au
waliojiajiri wenyewe, wakiwemo wakulima, wavuvi, wafugaji, Boda boda na mama lishe, kujiunga na Mfuko kwa kuchangia
kima cha chini cha shilingi 20, 000 kila mwezi. “Fedha hizo unaweza kuzitoa kwa
mkupuo au kwa awamu kulingana na uwezo wa mwanachama,” alifafanua Sendegeya.
Akielezea
faida za kuwa mwanachama, Meneja huyo alisema, “Mwanachama atafaidika na fao la
Afya ambapo atapatiwa bima ya afya kupitia NHIF baada ya kuchangia shilingi
elfu 60,000 tu.” Alisema na kuongeza kuwa faida nyingine ni pamoja na
mwanachama kujipatia mkopo wa maendeleo ambapo sharti kuu la kupata mkopo huu
ni mwanachama kuchangia Mfuko kwa kipindi cha miezi sita, mkopo wa elimu,
lakini pia fao la uzeeni, alisema Meneja huyo.
Kuhusu
namna mwanachama anavyoweza kuchangia baada ya kujiunga na Mpango huo, Meneja
Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele alisema, “Kuna njia rahisi ya kuwasilisha
michango, ambayo ni kutumia mitandao ya simu, Airtel Money, Tigo Pesa na
M-Pesa.” Alisema.
Baadhi
ya wanakijiji waliojiunga na Mpango huo, wameipongeza PPF kwa kutoa elimu
ambayo imewafanya wajiunge na Mfuko huo na ni matarajio yao utasaidia kuboresha
shughuli zao.
“Mimi
ni mfuga nyuki, kilichonivutia ni jinsi Mfuko huu unavyoweza kutoa mikopo ya
maendeleo,” alisema Erasto Joseph, ambaye pia ni mwalimu wa shule.
Naye
Ishara Ibrahim ambaye ni mkulima, alisema, ni matarajio yake kuwa kujiunga na
PPF, basi ataweza kumudu kupata huduma ya afya kupitia Bima ya Afya.” Alisema.
Zawadi Hamza Sule, akionyesha kadi yake baada ya kukabidhiwa
Seif M. Mgumba akionyesha kadi yake ya uanachama wa PPF, kupitia Wote Scheme
Khadija R. Kitango, akionyesha kadi yake
Meneja wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya, akizungumza na wanachama hao wapya wa PPF huko Ikwiriri, wilayani Rufiji mkoa wa Pwani Oktoba 3, 2016
Wanachama wapya wa PPF, wakiwasikiliza viongozi wa PPF
Wanachama hawa wapya wakionyeshana kadi zao za uanachama baada ya kukabidhiwa
Wanachama wakisubiri utaratibu wa kukabidhiwa kadi zao na kufanya malipo ya michango ya awali
Wanachama wapya wa PPF, wakihudumiwa.
Meenja wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica (kushoto), na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Mengele, wakiwasaidia wanachama hao kutumia simu zao za mkononi kuweka michango yao
Erica, akiwasaidia kuwaelekeza namna ya kutuma michango kupitia simu za mkononi
Erica (kulia) na Lulu, wakimsikiliza mwanachama huyu wa Ikwiriri baada ya zoezi la kuwapatia kadi za uanachama Oktoba 3, 2016
Erica, akisoma majina ya wanachama wapya waliojiunga na PPF kupitia Wote Scheme
Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele, akiwaarifu waandishi wa habari kuhusu shughuli nzima ilivyokwenda
Lulu akisalimiana na wanachama hawa wenye furaha
Wanakijiji wa Ikwiriri wakisubiri kupatiwa kadi zao za uanachama baada ya kujiunga na PPF kupitia uchangiaji wa Hiari, (Wote Scheme) Oktoba 3, 2016.
No comments:
Post a Comment