Timu
za soka za Simba na Yanga za Jijini Dar es Salaam zimezuiwa kutumia Uwanja wa
Taifa kwa muda usiojulikana kutoka na mashabiki wao kusababisha uharibifu wa
miumbombimu ya Uwanja wa Taifa yakiwemo
mageti ya kuingilia Uwanjani na kung’oa viti kwa upande wa mashabiki wa Simba.
Uamuzi
huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam
na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa
akikagua na kutembelea maeneo
yalioathirika na uharibifu uliofanywa na
mashabiki wa Simba na Yanga katika mechi iliyochezwa Octoba mosi 2016 katika
Uwanja wa Taifa.
“Hii
si mara ya kwanza kwa mashabiki kuvunja mageti na kung’oa viti na sisi kama
Serikali tumeamua kuzuia vilabu hivi vya Simba na Yanga kutotumia Uwanja wa
Taifa mpaka tuitavyoamua vinginevyo hapo baadae” Alisistiza Mhe. Nnauye.
Mhe.
Nape Nnauye ameongeza kuwa wameendaa mfumo wa kutumia kamera Uwanjani ili
kubaini makosa yatakayokuwa yanafanyika ili kuzuia vitendo vya kihualifu na
uharibifu katika Viwanja vya michezo.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex
Nkenyenge amesema kuwa wamesikitishwa sana na uharibifu ulitokea katika mechi
ya Simba na Yanga na kusababisha uharibifu wa viti na mageti ya kuingilia Uwanjani.
Ameongeza
kuwa kwa tathimini iliyofanyika mageti manne yameng’olewa na mashabiki kwa
upande wa Simba na Yanga na pia kwa upande wa ndani jumla ya viti 1781
vimeng’olewa katika upande wa mashabiki wa Simba.
“Mara
nyingi tumekubaliana kutunza Uwanja huu kwa ajili ya matumizi ya watanzania
wote na kama wasimamizi tunasikitika kwa kitendo hiki kilichotokea na tujue
kuwa ni kodi za wananchi ndio zilitumika kujenga Uwanja huu na pia ndizo
zitazotumika kukarabati uwanja tuwe na tabia ya kupenda na kutunza vya kwetu.
Klabu
za Simba na Yanga zimekuwa na ushindani mkubwa katika soka la Tanzania na
kumekuwa kukitokea mambo mbalimbali pale timu hizo zinapokutaana ikiwemo
uharibifu wa miundombinu katika Viwanja na vurugu kwa mashabiki pale mmoja wao
anapofungwa.
No comments:
Post a Comment