HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 02, 2016

NHC YAKABIDHI MARARASA SHULE YA MSINGI SAKU WILAYA YA TEMEKE

1
Meya wa Halmashauri ya Temeke Abdallah Chaurembo akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa madarasa ya shule ya msingi Chamazi Saku wilayani Temeke wakati wa makabidhiano yaliyofanyika shuleni hapo jana, Madarasa hayo yamejengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC kwa gharama ya shilingi milioni 32 , makabidhiano hayo yamefanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Nassib Mmbaga , Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Shirika la Nyumba NHC Susan Omari na Mkuu wa wilaya ya Temeke Mh. Felix Lyaviva.
2
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Shirika la Nyumba NHC Susan Omari akifungua mlango mara baada ya makabidhiano hayo kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw. Nassib Mmbaga na kushoto ni Meya wa Halmashauri ya Temeke Abdallah Chaurembo.
3
Haya ndiyo madarasa yaliyojengwa na Shirika la Nyumba NHC kwa gharama ya shilingi Milioni 32 katika shule ya msingi Chamazi Saku.
5
Baadhi ya wanafunzi wakikokotoa hesabu walizopewa na Mh. Meya wa Manispaa ya Temeke Halmashauri ya wilaya ya Mh. Temeke Abdallah Chaurembo.
6
Mh. Meya wa Halmashauri ya wilaya ya Temeke Abdallah Chaurembo akiwafundisha hesabu wanafunzi wa darasa la sita katika shule ya ya msingi Chamazi Saku.
7
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Shirika la Nyumba NHC Susan Omari akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake mara baada ya makabidhiano ya madarasa hayo.
8
Mh. Meya wa Manispaa ya Temeke Halmashauri ya wilaya ya Mh. Temeke Abdallah Chaurembo akikabidhi vitabu kwa mwanafunzi Leokadia Projestus wa darasa la sita shule ya msingi Chamazi Saku katikati ni Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Shirika la Nyumba NHC Susan Omari
9
Mkuu wa wilaya ya Temeke Mh. Felix Lyaviva. akizungumza na wanafunzi.
11
mwanafunzi Leokadia Projestus wa darasa la sita shule ya msingi Chamazi Saku akitoa hotuba kwa niaba ya wanafuzni wenzake.

No comments:

Post a Comment

Pages