HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 31, 2016

WAANDISHI WA HABARI DODOMA WATEMBELEA MIRADI YA UWEKEZAJI YA LAPF

Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Ramadhani Mkeyenge akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma, kuhusu miradi iliyotekelezwa na LAPF katika maeneo mbalimbali nchini. 
Maabara ya Kompyuta katika Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo. 
Baadhi ya Maofisa wa LAPF pamoja na waandishi wa Habari wakitembelea mradi wa mabweni katika Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo nje kidogo ya manisapaa ya Dododma. LAPF imetumia bilioni 39 kujenga baadhi ya majengo na miundombinu katika chuo hicho. 
Mradi wa Mabweni katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) LAPF imetumia bilioni 22 kujenga majengo na miundombinu katika Chuo cha Elimu ya Tiba na Afya chuoni hapo kwa awamu ya kwanza ya mradi huo.
Moja ya Vyumba vya madarasa katika Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo 'Sehemu ya mradi wa LAPF'. Darasa hili lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 520 kwa wakati mmoja.

No comments:

Post a Comment

Pages